• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mpwapwa District Council
Mpwapwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
        • Fedha
        • Biashara
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Mali asili
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Usafi na Mazingira
      • Utawala na Utumishi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Habari Mawasiliano na Tehama
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
    • Mamlaka
      • Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mpwapwa
      • Mamlaka ya Maji Mpwapwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashuri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa mbali mbali
    • Fomu za Maombi
    • Miongozo mbali mbali
    • Simulizi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video mbali mbali
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Education


 Elimu Sekondari

Wilaya  ina jumla ya Shule   za Sekondari 26 zenye jumla ya wanafunzi 8,405 na walimu 362 Kati ya shule hizo, 24 ni za Serikali na kuna Shule 2 za watu  binafsi ambazo husomesha wanafunzi waliokosa nafasi katika Shule za sekondari za serikali.

Idara ya Elimu Sekondari ni moja kati ya Idara kumi na tatu (13) za Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa. Idara ya Elimu Sekondari ina jumla ya  vitengo viwili ambavyo ni Kitengo cha Taaluma na Kitengo cha Vifaa na Takwimu. Aidha Idara ina jumla ya watumishi 443 ambapo watatu kati yao ni Maafisa katika Idara.Takwimu halisi za watumishi hawa ni kama ifuatavyo:-

NA
ENEO LA KAZI.
MAHITAJI
WALIOPO
UPUNGUFU

1

Maafisa ofisi ya Elimu Wilaya

3

3

0

2

Walimu masomo ya sayansi

173

75

98

       3

Walimu masomo ya sanaa

201

352

-151

4

Walimu wa masomo ya biashara

5

4

1

5

Wahasibu

24

1

23

6

Wahudumu

25

2

23

7

Makarani (PS)

25

1

24

8

Mafundi sanifu ( L/Tech )

24

0

24

9

Wakutubi

24

0

24

10

Wapishi shule ya bweni

5

2

3

11

Walinzi

24

2

22

12

Mganga shule ya bweni

1

0

1

13

Dereva

2

2

0

14

Walezi wa mabweni

6

0

6

15

Mafundi mchundo

24

0

24

16

Boharia

24

1

23


JUMLA

590

445

145

 

ORODHA YA WATUMISHI WA IDARA YA ELIMU SEKONDARI

 
Na
 
      Jina la Mtumishi
    
     Elimu
 
Mwaka wa Kuajiriwa
 
Umri kazini
 
Kitengo
1
Suma Mwampulo
Shahada ya Elimu

1999

18

Mkuu wa Idara

2
Coleman Andrew
Shahada ya Elimu

2007

10

Afisa Elimu Taaluma
3
Flora Mkwama
Shahada ya Elimu

1993

24

Afisa Elimu Vifaa na Takwimu


Idara inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Dira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ya kuwa Taasisi inayomjali mteja katika utoaji wa huduma kwa ajili ya maendeleo endelevu ifikapo 2025  na Mwelekeo wa kuwapatia wananchi wake huduma bora za kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia misingi ya utawala bora.

Hivyo Lengo kuu la Idara yetu ni kusimamia utoaji wa Elimu bora katika Halmashauri.

Majukumu ya Idara

Kitengo cha Taaluma

Majukumu ya kitengo cha Taaluma ni kama ifuatavyo-:

  1. kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa taarifa za ukaguzi wa shule za sekondari.
  2. kuratibu na kusimamia mitihani ya kitaifa inayoendeshwa kwa shule za sekondari  katika halmashauri .
  3. kubuni mipango  ya mitihani  ya elimu ya sekondari na kusimamia utekelezaji wake
  4. kuhakikisha kuwa walimu na watumishi wengine wa shule za sekondari wanafanyiwa tathimini ya wazi ya utendaji kazi open performance review and appraisal system-opras.
  5. Kubuni na kuratibu mipango ya mafunzo kazini  kwa walimu na watumishi wengine  kwa shule za sekondari
  6. Kuratibu  mashindano ya michezo na taaluma ya shule za sekondari katika halmashauri .
  7. Kuhakikisha walimu wa shule za sekondari  wanapangwa katika shule  kwa kuzingatia ikama inayokubalika
  8. Kusimamia kikamilifu  suala  la ufundishaji kwa kuhakikisha kuwa  walimu wantimiza majukumu yao ipasavyo.

 Kitengo cha Vifaa na Takwimu

Kitengo hiki kina majukumu yafuatayo;

  • Kuratibu, Kukusanya na kuchambua takwimu za Elimu ya Sekondari Katika Halmashauri
  • Kusimamia na kufuatilia ukarabati ,upanuzi na ujenzi wa shule za Sekondari
  • Kufanya Makisio ya mahitaji ya walimu kimadaraja na kimasomo
  • Kuagiza na kusambaza vifaa vya Shule kufuatana na mahitaji ya shule
  • Kufuatilia mapato na matumizi ya fedha katika shule za Sekondari
  • Kufuatilia utekelezaji wa utoaji huduma mbalimbali kwa wanafunzi
  • Kufanya kazi nyingine zitakazotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri au Afisa Elimu wa Sekondari wa Halmashauri.

Malengo ya Idara kwa Mwaka wa fedha 2017

Kwa mwaka wa fedha 2017  Idara ilijiwekea malengo yafuatayo;

 Kitengo cha Vifaa na Takwimu.

  • Kusimamia ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa katika shule ya sekondari Mbuga na Mima chini ya Mpango wa Maendeleo ya Sekondari (SEDEP II) ifikapo Juni 2017.
  • Kusimamia Ukamilishaji wa vyumba 4 vya madarasa katika shule ya sekondari ya Matomondo ifikapo 2017
  • Kusimamia Ujenzi wa matundu 24 ya vyoo katika shule ya sekondari Matomondo, Mbuga na Mima ifikapo Juni 2017.
  • Kusimamia Ujenzi wa nyumba 2 za Walimu katika shule ya sekondari Matomondo na Mbuga ifikapo Juni 2017.
  • Kusimamia ukarabati mdogomdogo katika majengo ya shule ifikapo Juni 30,2017

Malengo kwa mwaka wa fedha 2016/2017

  • Kitengo cha Taaluma
  • Kusimamia na kutembelea shule zote 26 za sekondari hadi ifikapo juni 2017 mara kwa mara kuhakikisha watahiniwa wanaandaliwa kikamilifu,ikiwemo kuweka kambi kuanzia mwezi aprili 2017.
  • Kuhakikisha wanafunzi wanahudhuria shuleni na wanafanya majaribio ya marakwa mara,na pia kupunguza utoro kwa asilimia 80% hadi ifikapo juni 2017.
  • Kuendesha mitihani ya majaribio ya mara kwa mara,kufanyika PRE MOKO NA PRE NATIONAL, kwa kidato cha pili na cha nne kabla ya septemba 2017.
  • Kumaliza mada zote za masomo kabla ya Oktoba mwaka huu.
  • Kuratibu maendeleo ya mwanafunzi mmojammoja  kwa kutumia fomu maalumu ya individual progress report,itakayo tumika pia kuwagawa wanafunzi katika makundi mbalimbali na kuwatumbua wanafunzi dhaifu ili  kuweza kuwaandalia maandalizi maalumu,hadi juni 2017.
  • Kuchukua  hatua kwa walimu wazembe watakaobainika kutokwenda na kasi ifikapo juni 2017.
  • Kuwepo na remedial classes kwa kidato cha Nne na cha pili hadi septemba 2017.
  • NB. Hatua za kinidhamu zimeanza kuchukuliwa kwa walimu wazembe.Walimu sita wa Ihala sekondari wameandikiwa barua za onyo kwa kosa la kuchelewa kazini na kutokuwa na maandalizi ya utendaji kazi.

 Kitengo cha Vifaa na Takwimu

  • Kusimamia Ukamilishaji wa vyumba 4 vya madarasa katika shule ya sekondari Mbuga na Mima chini ya Mpango wa Maendeleo ya Sekondari (SEDEP II) ifikapo Juni 2017.
  • Kusimamia Ukamilishaji ukarabati wa vyumba 4 vya madarasa katika shule ya sekondari ya Matomondo ifikapo Juni 2017
  • Kusimamia Ukamilishaji wa matundu 24 ya vyoo katika shule ya sekondari Matomondo, Mbuga na Mima ifikapo Juni 2016.
  • Kusimamia Ukamilishaji wa nyumba 2 za Walimu katika shule ya sekondari Matomondo na Mbuga ifikapo Juni 2016.
  • Kusimamia Kufanya ukarabati mdogomdogo katika majengo ya shule ifikapo Juni,2017
  • Kusimamia matumizi bora ya fedha shuleni


MPANGO KAZI WA IDARA

MPANGO KAZI WA IDARA KWA MWAKA 2017.

S/N
LENGO
KAZI ZITAKAZOTEKELEZWA

MUDA WAUTEKELEZAJI

 

1

Kuinua kiwango cha elimu kwa shule zenye matokeo dhaifu.
Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara shuleni

Januari - Novemba 2017.


2

Kuchukua hatua kwa walimu wazembe, wasiojituma  na watoro  adhabu stahiki.
Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara shuleni kwa kufuatatilia mahudhurio ya walimu kazini,na kufanya ukaguzi wakiutendaji kazi.

Januari-Novemba 2017


3

Kurekebisha ikama ya walimu katika Shule zote Wilayani ili kupunguza tatizo la ukosefu wa walimu katika shule nyingine.
Kupanga walimu wa ajira mpya kulingana na mahitaji ya Shule ili kurekebisha ikama.

Januari hadi Julai 2017


4

Kushughulikia madeni mbalimbali ya walimu.
Kuendelea kuwatambua walimu wenye madeni halali na kuwasilisha kwa mkaguzi mkuu wa ndani kuhakikiwa kwa lengo la kuingizwa katika orodha ya madeni.Kushugulikia fedha  za likizo kwa walimu wanao stahili kwenda likizo.

Januari   hadi Novemba 2017.


5

Kuratibu na kufuatilia ujenzi wa maabara tatu Kw akila Shule .
Kufuatilia kiasi cha michango inayotolewa na ya wananchi kwa kukaa na watendaji na Wakuu wa Shule kuendelea kuhamasisha ukusaji wa michango kwa lengo la kukuamilisha ujenzi huo

Januari   hadi Novemba 2017.


6

Kusimamia na kuendeleza michezo kwa  shule za sekondari
Kuhakikisha kuwa mashindano yanafanyika kama ratiba ilivyopangwa ikiwa ni pamoja kutoa motisha kwa kuboresha zawadi na vifaa bora vya michezo

Januari   hadi Novemba 2017.


7

Kusimia utekelezaji wa sera  ya elimu bila malipo
Kuhakikisha wanafunzi wote wa sekondari katika wilaya wanapata elimu bila malipo,ikiwa ni pamoja na kusimamia matumizi sahihi ya fedha za elimu bila malipo kulingana na miongozo ya wizara,pia kuhakikisha hakuna mchango wowote unaochangishwa shuleni bila kibali.

Januari   hadi Novemba 2017.


8

Kusimamia ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya shule
Kufuatilia na kukagua miundombinu ya Shule kama vyoo,madarasa na nyumba za walimu,kwa kuelekeza na kusimamia ukarabati wake ikiwa ni pamoja na kuratibu ujenzi wa majengo mapya.

Januari   hadi Novemba 2017.


9

Kutatua tatizo la madawati na vifaa vyakujifunza na kufundishia.
Kushiriana na wadau mbalimbali na Serikali ili kutatua tatizo la madawati. Pia kusimamia matumizi sahihi ya fedha za elimu bila malipo ili Kuhakikisha vifaa vya kutosha vinanunuliwa shuleni.

Januari   hadi Novemba 2017.


10

Kununua vitendea kazi bora vya ofisi.
Kuomba fedha kwa ajili ya kununua vitendea kazi vya idara kama compyuta 2 na printer 2 ili kuboresha utendaji kazi wa idara

Januari   hadi Novemba 2017.


11

Kuratibu usajili wa watahiniwa wa kidato cha Nne na cha Pili .
kugawa vifaa vya usajili kwa watahiniwa wa mtihani wa taifa wa kidato cha pili na cha nne kwa Wakuu wa Shule na kutoa maelekezo ya usajili .

Januari  2017 hadi machi  2017.








 

    HALI  YA UFAULU

Katika  matokeo ya mtihani wa taifa kwa kidato cha nnne mwaka 2016 . Asilimia 60% ya watahiniwa  wamefaulu mtihani huo kwa daraji la kwanza hadi la nne kati ya watahiniwa 1539 waliofanya mtihani huo.Aidha ufaulu huu ni sawa na ongezeko la asilimia 11.76 ukilinganisha na 48.24 % ya wanafunzi waliofaulu mwaka jana kati ya watahiniwa 1565 waliofanya mtihani.

Aidha kidato  cha pili  93% ya wanafunzi wote 1757  waliofanya mtihani wa upimaji wa kitaifa  wamefaulu kuendelea na kidato cha tatu ,ukilinganisha na asilimia 91.3% ya wanafunzi 1506 waliofanya mtihani mwaka jana 2015.

Ufaulu huu umetokana na mikakati iliyowekwa na kitengo cha taaluma kwa mwaka jana ikiwemo kusimamia ufundishaji, na mitihani ya mara kwa mara ya kuwapima watahiniwa wa kidato cha pili na cha Nne.

Kiambatanisho A na B vinaonesha matokeo ya mitihani ya kitaifa kwa miaka sita kwa kidato cha pili na Nne toka 2011 hadi sasa.

 Vitendea Kazi.

Pamoja na upungufu wa vitendea    idara inavyo vitendea kazi kama ilivyoorodheshwa katika jedwali hapo chini;

NA

AINA YA KIFAA

IDADI

HALI YA KIFAA

1

MEZA 

5

NZIMA ZINATUMIKA

2

VITI  VYA MBAO

15

VIZIMA VINATUMIKA

3

VITI  (EXCUTIVE)

2

KIMOJA  KINATUMIKA NA KIMOJA NI KIBOVU

4

CABINET

4

NZIMA ZINATUMIKA

5

SHELFU ZA MBAO

4

NZIMA ZINATUMIKA

6

MIHURI

12

MIZIMA

7

FIRE EXTINGUISHER

1

NZIMA ZINATUMIKA

8

COMPUTER  (DESK TOP)

1

NZIMA INATUMIKA

9

LAP TOP

3

MBILI NZIMA ,MOJA NI MBOVU

10

HARD DISK

1

NZIMA INATUMIKA

11

GARI LANDCRUISER

1

NZIMA INATUMIKA

12

BENCHI ZA KUKALIA

2

NZIMA ZINATUMIKA

13

PRINTER

1

NZIMA  INATUMIKA

14

PHOTOCOPY MACHINE

1

NZIMA INATUMIKA

 

Miundombinu

Na
Aina
Mahitaji
Yaliyopo
Upungufu/Ziada

1

Madarasa
384
268
116

2

Vyoo vya walimu
48
32
16

3

Vyoo vya wanafunzi
385
315
70

4

Maabara
72
10
62

5

Nyumba
372
106
266

6

Jiko
4
1
3

7

Hosteli
48
19
29

8

Maktaba
24
1
23

9

Jengola utawala
24
17
7

10

Madawati
8930
7821
1109

 

Vifaa vilivyopo havitoshi na hivyo vinaathiri sana utekelezaji wa majukumu, na vilivyopo vimeshakuwa vya muda mrefu na hivyo kuhitaji matengenezo ya mara kwa mara, Idara imeweka katika mpango wa bajeti ya 2017/2018 kununua vifaa vya ofisi.

MAJUKUMU  YALIYOTEKELEZWA HADI SASA.

Kumekuwepo na zoezi la ukaguzi wa shule  kuanzia January mwaka huu na tayari  shule kumi na mbili  kati ya shule 25 za serikali zimefanyiwa ukaguzi yakinifu wa kitaaluma. Shule hizo ni Mazae,Mwanakianga,Vingawe,Mpwapwa,Mount igovu,Ihala,Chunyu,Kibakwe,Pwaga,Mtera,Chipogoro na Matomondo.

Aidha kaguzi huu uliwahusisha Maafisa wote Idara ya Elimu Sekondari,Katibu wa TSD Wilaya  na  mdhibiti Ubora wa Shule kutoka Idara ya Udhibiti Ubora Wilaya.

Lengo la ziara hizi ni kusimamia Taaluma, nakuwajengea uwezo walimu juu ya mbinu mbalimbali za ufundishaji.

Ukaguzi huu unaendelea  katika kuhakikisha kuwa shule zote zinakaguliwa.Shuguli zilizofanywa na idara kutoka januari hadi sasa ni kama ifuatavyo-:

  • Tathimini ya matokeo ya mitihani  ya kitaifa kwa kidato cha pili na cha nne kwa mwaka 2016. Aidha  Kila shule imeagizwa kufanya tathimini ya matokeo ya mitihani, ili kubaini sababu za ufaulu duni wa wanafunzi kwa mitihani ya kitaifa iliyofanyika mwaka jana .
  • Tathimini hii imefenyika kwa kila idara ,kwa idara za masomo yote  kwa   shule kumi na mbili zilizokaguliwa hadi sasa ,  sababu za ufulu duni zilizobainika katika shule hizi ni  -:
  • -Maandalizi duni ya watahiniwa,kwa kukosa mitihani ya mara kwa mara ya ndani -Baadhi ya walimu     kuchelewa kumaliza mada  za masomo kwa wakati  hivyo  kutofanyika kwa marudio.
  • Wanafunzi wengi kutoshiriki mitihani ya majaribio.
  • Utoro sugu na wareja reja  Kwa wanafunzi.
  • Kutokuwepo kwa  mkakati wa ufaulishaji kwa shule nyingi.
  • Mikakati iliyopo katika baadhi ya shule kutokutekelezwa.
  • Uzembe wa baadhi ya walimu kuchelewa kazini na  kutowajibika ipasavyo.
  • Bodi za shule kukosa mipango na mikakati ya kusimamia shule.
  • Ushirikiano duni wa wazazi kwa shule .
  • Wanafunzi kutokuwa na notes.
  • Wanafunzi wengi kuishi mbali na shule.
  • Katika kuhakikisha ufaulu unapanda zaidi  mwaka huu Idara katika idara ya Elimu Sekondari kimebuni mitihani mbalimbali ya kuwaandaa wanafunzi kwa kipindi cha mwaka huu. 
  • Mitihani ya PRE-NATIONAL iliyofanyika septemba mwaka jana kwa kidato cha nne, ilisaidia sana katika kuongeza ufaulu.
  • Aidha  kwa mwaka  huu utafanyika mtihani wa PRE-MOKO,na PRE –national  Kwa vidato vya pili na nne ikiwa ni moja ya mkakati wa kuinua ufaulu,pia  tutakua na mitihani ya ujirani mwema ,sambamba na  mpango wa kuomba kibali cha wanafunzi kuchangia mitihani hii ya kujipima.

 

Jedwali Na 11: Hali ya miundombinu shule za Sekondari Januari, 2016

S/N
Aina
Mahitaji
Yaliyopo
Upungufu
1
Madarasa

225

268

-

2
Nyumba za  Walimu

372

91

281

3
Matanki ya kuvunia maji ya mvua

24

4

20

4
Matundu ya vyoo Wanafunzi

374

291

83

5
Matundu ya vyoo Walimu

48

26

22

6
Maktaba

24

1

23

7
Bwalo

24

1

23

8
Stoo

35

5

30

9
Hostel

78

19

59

10
Majengo ya Utawala

24

17

7

11
Jiko

24

1

23

12
Maabara

75

6

69

13
Solar

18

0

18

14
Madawati

7,694

7,694

1,130


Suma Mwampulo- Mkuuwa Idara

Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usahili MpwapwaDC June 27, 2022
  • Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa May 2022 May 31, 2022
  • Tangazo la kuahirishwa kwa Usahili Halmashauri ya Mpwapwa June 22, 2022
  • Tangazo la Kuahirishwa kwa kikao cha Kamati ya Fedha uongozi na Mipango March 31, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mgao wa Pikipiki Kwa Watendaji wa Kata

    March 01, 2023
  • Mtokeo ya kidato cha nne yatangazwa

    January 29, 2023
  • Matokeo ya Mtihani Darasala nne na Kidato cha Pili 2022

    January 04, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Saba yatangazwa

    December 01, 2022
  • Tazama zote

Video

Video ya Mpango wa Uuzaji wa Viwanja Eneo la Mazae Block "E" katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa -2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
  • Muundo wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani
  • Ratiba ya Vikao vya Madiwani

Viunganishi Linganishi

  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Utumishi portal
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu Teknolojia na Sayansi
  • Sekretarieti ya Ajira

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mpwapwa - Dodoma, Tanzania

    Anwani: S.L.P 12

    Simu: 255 26 2320122/2320

    Simu ya Kiganjani: +255 688639341

    Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovutii

Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.