• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mpwapwa District Council
Mpwapwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
        • Fedha
        • Biashara
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Mali asili
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Usafi na Mazingira
      • Utawala na Utumishi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Habari Mawasiliano na Tehama
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
    • Mamlaka
      • Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mpwapwa
      • Mamlaka ya Maji Mpwapwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashuri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa mbali mbali
    • Fomu za Maombi
    • Miongozo mbali mbali
    • Simulizi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video mbali mbali
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Wizi wa punda watishia kuongezeka kwa kiwango cha umasikini Walayani Mpwapwa

Thursday 23rd, March 2023
@Mpwapwa

Serikali imeobwa kuweka mkakati maalum wa kudhibiti wimbi la uwizi wa punda unaotokana na kukithiri kwa uhitaji wa ngozi ya Punda, kutokana na mnyama huyu kuwa katika hatari kubwa ya kutoweka nchini na hivyo kusabisha kuongezaka kwa wimbi la umaskini kwa jamii nyingi za vijijini zinazo mtegemea mnyama huyu kwa shughuli  mbalimbali ikiwemo kubeba mizigo..
Matukio ya uwizi wa punda yamekuwa yakiongeeka kila kukicha sehemu  mbalimbali za wilaya ya Mpwapwa na mkoa mzima wa Dodoma. Katika Tukio lililotokea katika kijiji Mzase kata ya Berege wilayani hapa punda watano wamekutwa wameibwa na kuchunwa ngozi huku mizoga yao ikiwa ametelekezwa porini. 

Mmoja wa wanakijiji hicho bwana Naftari Asheri amesema kuwa endapo jitihada za makusudi hazitachukuliwa za kuweza kuokoa wizi wa punda kuna uwezekano mkubwa wa wanyama hao kutoweka na na hivyo kusababisha ongezekao la umaskini sehemu za vijijini kulingana na umuhimu wa mnyama huyo katika maisha ya Mtanzania.  Aidha Bwana Naftari alisema kuwa lazima serikali iweke mkakati madhubuti wa kukabiliana na changamoto ya kumuokoa mnyama huyo ambae siku za hivi karibuni amekuwa akiwindwa zaidi kuliko mnyama yoyote yule.

Mkurugenzi wa shirika la TAWESO Dkt. Kahema alisema kuwa kutokana na kuzidi kushamili kwa biashara hii ya ngozi za punda katika jamii kunatishia wanyama hawa kuzidi kupungua siku hadi siku na kusababisha kupungua kwa nguvu kazi ya mfugaji wa punda kila kukicha. Aidha Dkt Kahema alisema kutokana na utafiti uliofanywa na shirika hilo imebaini kuwa kila siku punda zaidi ya mia moja wanauwawa kila siku kwa kuchinjwa kama kitoweo au kwa ajili ya kuuza ngozi yake katika viwanda vya wachina vilivyoko Dodoma na Shinyanga na katika jamii. Alisema kuwa kama jitihada za makusudi hazitachukuliwa ndani ya miaka mitatau mbeleni taifa litakuwa halina mnyama kazi kama punda kutokana na biasahara ya ngozi yake kushika kasi sana katika bara la Asia hasa nchini China. 

Hata hivyo Dkt Kahema alisema kuwa kwa sasa Tanzania inakadiliwa kuwa na punda wasio zidi laki tano nchi nzima lakini uwiano wa uzalishaji na uchinjaji wa Punda kwa siku haviendani na kutishia mnyama huyo kutoweka kabisa katika jamii. Alidai kuwa Punda amekuwa akifanya kazi za kila siku za mwananchi wa hali ya chini kijijini hivyo mnyama huyo akipotea basi wimbi la umaskini litaongezeka hapa nchini. “ Unajua kwa sasa punda mzima anauzwa kwa shilingi laki mbili wakati kwa mwaka punda anafanya kazi za zaidi ya milioni tano kwa mkulima kama kulima, kuchota maji, kubeba mizigo na shughuli zote za kila siku kwa mkulima” aliongea Dkt Kahema.
Alisema kutokana na ugumu wa maisha ya mnyama huyu uzalishaji wake kwa mwaka umekuwa wa shida ambapo punda hubeba mimba kwa miezi 12 na  huingia joto mara baada ya miaka mitatu hivyo huzalishaji wake umekuwa ni mdogo sana ukilinganishwa na upoteaji wake katika jamii. Katika kipindi cha miezi sita punda zaidi ya 27 walichunwa ngozi na mizoga yao kutelekezwa,   matukio hayo yalilipotiwa katika kituo cha polisi na kesi zikiwa zikiendelea katika mahakama mbalimbali hapa wilayani hapa

                         Mizoga ya punda ikiwa imetelekezwa porini katika kijiji cha Mazase kata ya Berege

Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usahili MpwapwaDC June 27, 2022
  • Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa May 2022 May 31, 2022
  • Tangazo la kuahirishwa kwa Usahili Halmashauri ya Mpwapwa June 22, 2022
  • Tangazo la Kuahirishwa kwa kikao cha Kamati ya Fedha uongozi na Mipango March 31, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mgao wa Pikipiki Kwa Watendaji wa Kata

    March 01, 2023
  • Mtokeo ya kidato cha nne yatangazwa

    January 29, 2023
  • Matokeo ya Mtihani Darasala nne na Kidato cha Pili 2022

    January 04, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Saba yatangazwa

    December 01, 2022
  • Tazama zote

Video

Video ya Mpango wa Uuzaji wa Viwanja Eneo la Mazae Block "E" katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa -2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
  • Muundo wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani
  • Ratiba ya Vikao vya Madiwani

Viunganishi Linganishi

  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Utumishi portal
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu Teknolojia na Sayansi
  • Sekretarieti ya Ajira

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mpwapwa - Dodoma, Tanzania

    Anwani: S.L.P 12

    Simu: 255 26 2320122/2320

    Simu ya Kiganjani: +255 688639341

    Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovutii

Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.