• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mpwapwa District Council
Mpwapwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
        • Fedha
        • Biashara
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Mali asili
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Usafi na Mazingira
      • Utawala na Utumishi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Habari Mawasiliano na Tehama
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
    • Mamlaka
      • Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mpwapwa
      • Mamlaka ya Maji Mpwapwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashuri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa mbali mbali
    • Fomu za Maombi
    • Miongozo mbali mbali
    • Simulizi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video mbali mbali
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana

USURI WA IDARA

UTANGULIZI:

Idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana ni miongoni mwa Idara na Vitengo 19 vinavyouunda Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

Idara ina jukumu la kuwasaidia wananchi binafsi au katika makundi kuelewa uwezo wao katika kutambua changamoto au mahitaji yao ya kimaendeleo au uwezo wao katika matumizi ya fursa na raslimali zinazopatikana katika maeneo yao katika kutatua changamoto hizo za kimaendeleo ili kujipatia kipato na kujiletea maendeleo na kuimarisha kiwango cha maisha kwa njia ya kujitegemea na msaada kutoka Serikalini na kwa wadau wa maendeleo.

MATARAJIO/NIA YA IDARA

Kuwawezesha wananchi kuelewa uwezo wao katika kuainisha changamoto, kuchambua na kutafuta utatuzi wa changamoto hizo kwa kutumia uwezo walionao na raslimali zinazopatikana katika maeneo

kuwawezesha wananchi wenye raslimali (ardhi, mifugo n.k) zitumike kubadilisha mfumo wao wa maisha kimaendeleo

Kuwahimiza wananchi kuanzisha vikundi vya kiuchumi vya wanawake, vijana, watu wenye ulemavu,  na makundi mengine kwa madhumuni ya kupambana na umasikini

Kuimarisha kanuni za utawala wa bora katika Halmashauri za Vijiji

kuelimisha jamii kuondokana mila, desturi na imani zinazokwamisha au zuia maendeleo

Kuongeza uelewa wa jamii na wananchi walio wengi juu ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI

MUUNDO WA IDARA 

Idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana imegawanyika katiak Vitengo vitatu (3), sehemu nne (4) na inasimamia programu nne (4) kama ifuatavyo:

A.VITENGO NA SEHEMU

     1.0 Kitengo cha Maendeleo ya Jamii

          1.1 Jinsia na Maendeleo

          1.2 Maendeleo ya Vijana

          1.3 Uratibu wa Asasi Zisizo za  Kiserikali (AZAKI)

          1.4 Ufundi, Ujenzi na Teknolojia

       2.0 Kitengo cha Ustawi wa Jamii

       3.0 Kitengo cha Maendeleo ya Vijana

  B. PROGRAMU ZA IDARA

      1.0 Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)

        2.0 Udhibiti UKIMWI

        3.0 Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)

        4.0 Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (Dawati)

HALI YA WATUMISHI

  Ili idara iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo kulingana na miundo ya Utumishi iliyopo inatakiwa kuwa na   watumishi wapatao 209, waliopo kwa mwaka 2016/17 ni 18 na upungufu ni 191 kwa mchanganuo ufuatao:

NA
KADA/CHEO
MAHITAJI
WALIOPO
UPUNGUFU
1
Mkuu wa Idara

1

1

0

2
Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Vijiji

113

0

113

3
Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Kata

33

4

29

4
Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Wilaya (desk officers)

10

10

0

5
Maafisa Ustawi wa Jamii ngazi ya Wilaya (desk officers)

13

2

11

6
Maafisa Ustawi wa Jamii Wasaidizi Kata

33

0

33

7
Maafisa Maendeleo ya Vijana    

2

0

2

8
Mafundi Sanifu

4

1

3

 
JUMLA
209
18
191

 

MALENGO, WAJIBU NA MAJUKUMU YA IDARA

Malengo ya Idara

Idara ina malengo makuu ainishi matatu ya Kuboresha huduma na kupunguza maambukizi ya VVU/ UKIMWI, Utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na vitendo vya Rushwa pamoja na kuboresha Ustawi wa Jamii, Jinsia, na kuwezesha jamii katika Maendeleo

Wajibu na Majukumu makuu ya Idara

Kuhamasisha na kuwezesha jamii kupanga na kutekeleza shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo

Kusaidia utayarishaji wa mipango ya jamii/wananchi kwa kutumia mbinu mpya ya Jitihada za Jamii yenyewe (Community Initiatives)

Kuwezesha jamii kuunda vikundi vya ujasiria mali, kiuchumi na kijamii

Kuhamasisha jamii juu ya masuala ya jinsia na maendeleo

Kuunganisha wadau mbalimbali katika shughuli za maendeleo

Kuhamasisha jamii katika kukabiliana na maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI

Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa shughuli mbalimbali chini ya Programu za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Udhibiti UKIMWI, Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) na Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

Kuandaa na kutoa elimu na mafunzo mbalimbali kwa vikundi, jamii juu ya ujasiriamali, utawala bora na Haki za binaadamu

SERA MBALIMBALI ZA IDARA

Katika utekelezaji wa wajibu na majukumu ya Idara inazingatia Sera zifuatazo za Kisekta:

A: Sera ya Maendeleo ya Jamii ya 1996

 Lengo kuu la sera hii ni kuiwezesha jamii, watu binafsi,familia, vikundi, Asasi za Kiraia (AZAKI) na wadau wengine kuchangia zaidi kwenye nia na juhudi za Serikali ya kuinua ari kujitegemea na kuleta maendeleo katika ngazi zote

B: Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya 1996

Lengo kuu la Sera hii ni kuhakikisha kuwa kila Mtoto anapata haki zake za msingi zikiwemo:

  • haki ya kuishi
  • Haki ya kulindwa
  • Haki ya kupata elimu
  • Haki ya kushiriki kwenye maamuzi yanayomhusu
  • Haki ya kutokubaguliwa

C: Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya 2000

     Lengo kuu la Sera hii ni kuanzisha mazingira mazuri kwa        wanawake na wanaume kutimiza wajibu wao katika jamii na         kuondoa tofauti za ushiriki wa wanawake katika masuala ya         maendeleo kwa     kujenga uwezo wao katika maamuzi na kutenda

D: Sera ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya 2001

 Lengo kuu la Sera hii ni kuanzisha mazingira mazuri yatawezesha  Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuendeleza na kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa jamii.

E: Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003

Madhumuni ya jumla ya sera ni kuhakikisha kuwa wazee wa Tanzania wanatambuliwa na kupewa fursa ya kushiriki katika mambo yanayohusu      maisha ya kila siku kwa manufaa ya Watanzania wote.  Aidha kuhakikisha kwamba wazee wanapata huduma zote muhimu na za msingi ambazo zitawawezesha kushiriki kwa ukamilifu katika maisha ya kila siku ya       Watanzania

F: Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya 2007

Malengo ya jumla ya Sera hii ni kuwasaidia, kuwawezesha na kuwaongoza vijana na wadau wengine katika utekelezaji wa masuala ya maendeleo ya    vijana

 

G: Sera ya Taifa ya Watu Wenye Ulemavu ya Mwaka 2004

 Lengo la Sera hii ni kuimarisha hali ya maisha ya watu wenye ulemavu  kwa kuwapa moyo (encourage) katika maendeleo ya watu wenye ulemavu,  kuwezesha familia zao, kufanya mapitio au marekebisho ya sheria ambazo  sio rafiki kwa watu wenye ulemavu, kuimarisha huduma zao, kuruhusu  watu wenye ulemavu kushiriki kwenye maamuzi na kushiriki utekelezaji wa shughuli muhimu katika jamii na kuruhusu familia za watu wenye ulemavu   na jamii kwa jumla kushiriki katika maamuzi ya shughuli rafiki kwa watu  wenye ulemavu.

H: Sera ya Taifa ya Uwezeshaji wananchi Kiuchumi ya 2004

Lengo la msingi la Sera hii ni kutoa mwongozo wa jumla utakaohakikisha   watanzania walio wengi wanafikiwa na fursa na kushiriki kikamilifu katika   shughuli za kiuchumi katika sekta zote za uchumi

I: Sera ya Taifa ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI ya 2001

 Lengo la jumla la Sera hii ni kuweka mfumo wa uongozi na uratibu wa    kitaifa wa mwitikio kwa virusi vya UKIMWI na ugonjwa wa UKIMWI

Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usahili MpwapwaDC June 27, 2022
  • Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa May 2022 May 31, 2022
  • Tangazo la kuahirishwa kwa Usahili Halmashauri ya Mpwapwa June 22, 2022
  • Tangazo la Kuahirishwa kwa kikao cha Kamati ya Fedha uongozi na Mipango March 31, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mgao wa Pikipiki Kwa Watendaji wa Kata

    March 01, 2023
  • Mtokeo ya kidato cha nne yatangazwa

    January 29, 2023
  • Matokeo ya Mtihani Darasala nne na Kidato cha Pili 2022

    January 04, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Saba yatangazwa

    December 01, 2022
  • Tazama zote

Video

Video ya Mpango wa Uuzaji wa Viwanja Eneo la Mazae Block "E" katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa -2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
  • Muundo wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani
  • Ratiba ya Vikao vya Madiwani

Viunganishi Linganishi

  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Utumishi portal
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu Teknolojia na Sayansi
  • Sekretarieti ya Ajira

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mpwapwa - Dodoma, Tanzania

    Anwani: S.L.P 12

    Simu: 255 26 2320122/2320

    Simu ya Kiganjani: +255 688639341

    Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovutii

Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.