• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mpwapwa District Council
Mpwapwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
        • Fedha
        • Biashara
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Mali asili
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Usafi na Mazingira
      • Utawala na Utumishi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Habari Mawasiliano na Tehama
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
    • Mamlaka
      • Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mpwapwa
      • Mamlaka ya Maji Mpwapwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashuri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa mbali mbali
    • Fomu za Maombi
    • Miongozo mbali mbali
    • Simulizi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video mbali mbali
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Baraza la Madiwani Laazimia Mazito

Posted on: June 14th, 2018

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa leo tarehe 14 Juni 2018 lafanya kikao cha Robo ya Tatu 2017/2018. Kikao hicho kimehudhuriwa na waheshimiwa madiwani wa kuchaguliwa na wa viti maalam, Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri, wageni waalikwa, kamati ya ulinzi na usalama, wakuu wa idara, wananchi, watendaji wa kata, maafisa tarafa.

Agenda zilizowasilishwa ni kufungua kikao, kuthibitisha agenda, kupitia na kuthibitisha muhtasari wa kikao kilichopita cha tarehe 8 Februari 2018, maswali ya papo kwa papo, taarifa ya kutoka kwa mkurugenzi mtendaji, taarifa kutoka kwa wenyeviti wa kamati za kudumu: (a) Kamati ya huduma za jamii, (b) Kmati ya Huduma za Uchumi (c) Kamati ya Kuthibiti UKIMWI na (d) Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango. Agenda zingine ni taarifa ya mwenyekiti, salamu toka serikali kuu na kufunga kikao.

Waheshimiwa madiwani wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya tatu 2017/2018 katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa (Picha. Na. Shaibu J. Masasi -Afisa TEHAMA Mpwapwa)

Katika taarifa za wenyeviti wa kamati za kudumu, maazimio mbalimbali yameazimiwa na kuwasilishwa mbele ya baraza kwa utekelezaji. Maazimia hayo ni kama yafuatayo:-

Kamti ya Huduma za Jamii: Kamati hii iinaundwa n a jumla ya Idara tano ambazo ni Afya, Maji, Elimu Msingi, Elimu Sekondari na MAendeleo ya Jamii na Vijana. Kamati hii ilifanya kikao chake cha kawaida cha robo ya tatu mnamo tarehe 29 Mei 2018. Mwenyekiti wa kamati ni Mhe. Joctan Cheliga, diwani wa kata ya Lumuma.

Kamati ilijadili taarifa za utekelezaji wa kila idara inayounda kamati hii. Baada ya majadiliano kamati imeshauri na kuazimia yafuatao:-

  1. Kamati imepokea taarifa kutoka idara ya Elimu Sekondari na kubaini kuwa kuna idadi kubwa ya wanafunzi wanaopewa mimba, na hiii linatokana na kuwa wanaowapa mimba wanafunzi wanapofikishwa mahakamani ili sheria ichukuwe mkondo wake, matokeo yake  watuhumiwa huachiwa huru kwa kuonekana hawana hatia kwa mujibu wa sheria. Hivyo kamati imependekeza kuwa waheshimiwa madiwani wasimamie suala hili katika maeneo yao ili kuhakikisha watuhumiwa wanachukuliwa hatua.
  2. Kamati pia imepokea taarifa toka bodi ya CHF ambapo kumefanyika maboresho katika mfuko wa Afya ya jamii (CHF) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kuleta mfumo mpya wa CHF iliyoboreshwa ili kuleta tija na ufanisi katika kuratibu na utoaji huduma ya mfuko wa Afya ya Jamii ili kufikia malengo ya Kitaifa ambapo kila kaya itachangia mfuko kwa kutoa kiasi cha Tshs. 30,000/= (Elfu thelathini tu). Taarifa hii imetoka Ofisi ya Rais - TAMISEMI ikielezea kwa kina juu ya waraka huu ambao utaanza kutumika tarehe 1 Mei 2018.

Kamti ya Huduma za Uchumi: Kamati ya hii inaundwa na idara tano nazo ni idara ya mifugo na uvuvi, idara ya kilimo, umwagiliaji na ushirika, idara ya ujenzi, idara ya ardhi na idara ya usafi na mazingira. Mwenyekiti wa Kati hii ni Mhe. Richard E. Maponda diwani wa kata ya Luhundwa.

Kamati hii ya uchumi ilikaa kikao chake cha kawaida mnamo tarehe 29 Mei 2018 na kuazimia yafuatayo:

  1. Wananchi waendelee kusisitizwa juu ya kuhifadhi mazingira (ardhi) katika eneo la SACCOS ya Matomondo lenye ekari 45 ambalo tayari limeathirika na mvua na hivyo kusababisha kuwepo kwa korongo.
  2. Viwekea taka viimarishwe ili kutatua tatizo la takataka kusambaa ovyo katika makazi ya watukwani huweza kupelekea kusababisha madhara kama magonjwa kwa jamii. Pia wafanyabiashara wathibitiwe ili wasitupe taka ovyo katika makorongo.
  3. Waheshimiwa madiwani wahamasishe wananchi juu ya chanjo ya kichaa cha mbwa kwani ugonjwa huo unaathiri sana binadamu.
  4. Halmashauri itenge kiasi cha fedha kutoka katika mapato ya ndani ili kuweza kuwafidia wenye viwanja na kisha walionunua viwanja hivyo waweze kuviendeleza.
  5. Pia kamati imeagiza kuwa katika kila taarifa ya robo ya mwaka mhandisi wa ujenzi awe natoa taarifa kuhusu majengo yote yaliyopo Mpwapwa, taarifa ioneshe majengo yaliyoibuliwa na nguvu za wananchi na hatua iliyofikiwa pamoja na yale ambayo bado hayajatekelezwa.

Baadhi ya wageni waalikwai wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya tatu 2017/2018 katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa (Picha. Na. Shaibu J. Masasi -Afisa TEHAMA Mpwapwa)

Kamti ya Huduma za Kuthibiti UKIMWI: Kamati ya hii inaundwa na idara mbili nazo ni idara ya Afya na idara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto. Mwenyekiti wa kamati hii ni Mhe. George O. Fume ambaye ni diwani wa kata ya Mpwapwa Mjini. 

Kamati hii ya ilikaa kikao chake cha kawaida mnamo tarehe 29 Mei 2018 na kuazimia yafuatayo:

  1. Kamati inaendelea kusisitiza kuwa mradi wowote kabla haujaanza kutekelezwa ni muhimu kukatolewa elimu juu ya kuthibiti maambukizi ya UKIMWI pia kwa wakandarasi wa miradi ya barabara inayoendelea katika halmashauri.
  2. Kuwepo na mkakati wa kuwaamasisha wanaume kujitokeza kupima UKIMWi kutokana na asilimia ya wanaume kuwachini katika upimaji wa UKIMWI tofauti na wanawake.
  3. Kuwasisitiza wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wanasiasa, na taasisi za kijamii kutoa elimu kwa wananchi ili kupunguza kiwango cha maambukizi mapya kutokana na ujio wa serikali kuu Dodoma.


Daktari Said Mawji (aliyesimama mbele) ambaye ni Mganga Mkuu wa Wilaya akisubiri kukabidhiwa zawadi maalum toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe.Jabir Shekimweri. Zawadi hiyo imeandaliwa na waheshimiwa madiwani baada ya kuridhishwa na kufurahishwa na utendaji kazi wa daktari  hiyo. Zawadi hiyo imetolewa katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya tatu 2017/2018 katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa (Picha. Na. Shaibu J. Masasi -Afisa TEHAMA Mpwapwa)

Kamti ya Huduma Fedha, Uongozi na Mipango: Kamati ya hii inaundwa na idara fedha na biashara, mipango na takwimu, kitengo cha sheria, ukaguzi wa ndani nakitengo cha manunuzi. Mwenyekiti wa kamati hii ni Mhe. Donati S. Nghwenzi ambaye ni diwani wa kata ya Massa. 

Kamati hii ya uchumi ilikaa vikao vitatu  tarehe 1 Machi 2018, 26 Machi 2018, 9 Juni 2018,  na kuazimia yafuatayo:

  1. Asilimia 20 itokanayo na mapato ya katika kata ziwasilishwe kwa wakati, kwa zile akaunti ambazo hazijahuishwa mkakati ufanyike kuwataka serikali ya vijiji kuzihuisha akaunti zao kwa kujaza "Vendor Form" ili kuweza kuingiziwa fedha zao.
  2. Kila kata iwekewe makadirio ya ukusanyaji wa matato ili kuwezesha kujua hali halisi ya ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usahili MpwapwaDC June 27, 2022
  • Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa May 2022 May 31, 2022
  • Tangazo la kuahirishwa kwa Usahili Halmashauri ya Mpwapwa June 22, 2022
  • Tangazo la Kuahirishwa kwa kikao cha Kamati ya Fedha uongozi na Mipango March 31, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mgao wa Pikipiki Kwa Watendaji wa Kata

    March 01, 2023
  • Mtokeo ya kidato cha nne yatangazwa

    January 29, 2023
  • Matokeo ya Mtihani Darasala nne na Kidato cha Pili 2022

    January 04, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Saba yatangazwa

    December 01, 2022
  • Tazama zote

Video

Video ya Mpango wa Uuzaji wa Viwanja Eneo la Mazae Block "E" katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa -2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
  • Muundo wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani
  • Ratiba ya Vikao vya Madiwani

Viunganishi Linganishi

  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Utumishi portal
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu Teknolojia na Sayansi
  • Sekretarieti ya Ajira

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mpwapwa - Dodoma, Tanzania

    Anwani: S.L.P 12

    Simu: 255 26 2320122/2320

    Simu ya Kiganjani: +255 688639341

    Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovutii

Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.