• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mpwapwa District Council
Mpwapwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
        • Fedha
        • Biashara
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Mali asili
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Usafi na Mazingira
      • Utawala na Utumishi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Habari Mawasiliano na Tehama
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
    • Mamlaka
      • Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mpwapwa
      • Mamlaka ya Maji Mpwapwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashuri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa mbali mbali
    • Fomu za Maombi
    • Miongozo mbali mbali
    • Simulizi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video mbali mbali
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Baraza la Madiwani Laazimia Mazito - Mpwapwa

Posted on: November 27th, 2019

(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa leo limefanya kikao cha Robo ya Kwanza ya Julai - Septemba Mwaka 2019/2020 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa. Kikao hicho kilichokuwa kinaongozwa na Mhe. Donati S. Nghwenzi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Massa, kimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri, Wabunge, waheshimiwa wa madiwani wa kata 33, wakuu wa idara, watendaji wa kata, maafisa tarafa toka katika taarafa 3 na wananchi hususani wa kata ya Mpwapwa Mjini.

Aidha katika kikao hicho Waheshimiwa Madiwani wameazimia kuwa; eneo la Mazae lipimwe ili kuweza kupata viwanja zaidi ya 1,000  ambapo viwanja hivyo vitauzwa kwa wananchi na hivyo kuiingizia Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa fedha nyingi zitakazotokana na uuzaji wa viwanja hivyo. Pia Maeneo ya Kata ya Mtera yapangwe kwa kufauta hadhi ya mji ili baadae kuweza kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo.

Samabamba na hilo, Baraza hilo limeazimia kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ikamilishe miradi viporo kama vile Zahanati, Mdarasa na Mradi wa Mfereji wa Umwagiliaji katika Kiijiji cha Mafene kata ya Lumuma.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Nghwenzi amewasilisha taarifa yake na kusema kuwa "Katika mwaka wa fedha 2019/2020 Halmashauri ilipanga kukusanya Tsh. Bilioni 2.2 na kwa robo ya kwanza ya Julai - Septemba 2019/2020 ilipanga kukusanya Milioni 550 na kukusanya mapato halisi ya shilingi Milioni 433 hivyo kushindwa kufikia lengo". Sababu ya kutofikia lengo ni kutoka na hali mbaya ya hewa na kusababisha kupungua kwa mazao ya kilimo, usimamizi hafifu wa vyanzo vya mapato. Hivyo ameagiza kuwa jitihada zifanyike katika kukusanya vyanzo hivi kikamilifu.

Mhe. Nghwenzi, ameorodhesha miradi mbalimbali iliyotekelezwa katka Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, ikiwemo miradi ya maji 10 kuwa:  Mzase, Iyoma, Kidenge, Seluka,  Kingititi, Chogora, Bumila, Mima, Kibakwe na Mpwanila ambapo miradi hii mingi haitoi maji na kufanya adha kubwa kwa wananchi kutafuta huduma ya maji, hivyo ameziagiza mamlaka husika kufuatilia miradi hii na kutatua changamoto zilizopo. Pia ametaja jumla ya fedha zilizotolewa kwa miradi ya Maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ni Shilingi Bilioni 4.29 na zilizotumika ni Tsh. Bilioni 1.348, hivyo zingine bado hazijatolewa shilingi Bilioni 2.84.

Aidha Mhe. Nghwenzi, amewasilisha taarifa ya Vituo vya Afya vya Mima, Kibakwe na Pwaga, ambapo vituo vya Pwaga na Kibakwe vinafanyakazi japo havijakamilika. Kutokana na usimamizi mbovu wa vituo hivyo imepelekea kutokamilika kwa vituo kwa wakati na kusababisha harasa kwa serikali, hii ni kutoka na na kuongezeka kwa majengo ya wagonjwa wa nje (OPD) Kibakwe na Pwaga kumesababisha kuongezeka kwa gharama na kutomalizika majengo kwa kuwa majengo ya wagonjwa wa nje (OPD) hayakuwepo na katika mwaongozo (ramani) uliotolewa na Serikali. Pia ameongeza kuwa Ushauri wa Kujenga jengo la OPD ulitolewa na wataalam wa Halmashauri akiwemo Mhandisi wa Ujenzi wa Wilaya na Mganga Mkuu wa Wilaya.
Waheshimiwa madiwani wakifuatilia kwa makini mjadala na mada zinazowasilishwa katika Kikao cha Baraza la Madiwani Mpwapwa


Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri akitoa salam toka Serikali Kuu amesema kuwa "Viongozi wote wa Wilaya tufanye kazi kwa bidii na kwa kushiriana kuanzia Waheshimiwa madiwani, Kamati ya Ulinzi na Usalama  pamoja na watumishi wote kwa ujumla" Ameongeza kuwa "Afisa Utumishi unawajibu wa kukaa na watumishi hawa na kujua changamoto zao pamoja na kuwaelekeza kazi zao vizuri na kufuata sheria,  ninayasema yote haya kwa kuwa kama watumishi wakiwa wanaishi kwa amani katika mahali pa kazi hivyo usimamizi wa miradi itakuwa inasimamiwa vizuri. Pia naamini kuwa watumishi hawa wanakiu kubwa ya kuongea na mwajiri wao ili waseme mahusiano yanavunjika wapi ili kutatua changamoto zao".

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri (kushoto) akitoa salam toka Serilkali Kuu katika Kikao cha Baraza la Madiwani

Akifunga kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, amesisitiza kuwa Idara husika kufanyia kazi maazimio yote yaliyotolewa katika kikao hicho cha baraza la Madiwani ili kuweza kuwapatia wananchi huduma zinazostahili.

Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usahili MpwapwaDC June 27, 2022
  • Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa May 2022 May 31, 2022
  • Tangazo la kuahirishwa kwa Usahili Halmashauri ya Mpwapwa June 22, 2022
  • Tangazo la Kuahirishwa kwa kikao cha Kamati ya Fedha uongozi na Mipango March 31, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mgao wa Pikipiki Kwa Watendaji wa Kata

    March 01, 2023
  • Mtokeo ya kidato cha nne yatangazwa

    January 29, 2023
  • Matokeo ya Mtihani Darasala nne na Kidato cha Pili 2022

    January 04, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Saba yatangazwa

    December 01, 2022
  • Tazama zote

Video

Video ya Mpango wa Uuzaji wa Viwanja Eneo la Mazae Block "E" katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa -2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
  • Muundo wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani
  • Ratiba ya Vikao vya Madiwani

Viunganishi Linganishi

  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Utumishi portal
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu Teknolojia na Sayansi
  • Sekretarieti ya Ajira

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mpwapwa - Dodoma, Tanzania

    Anwani: S.L.P 12

    Simu: 255 26 2320122/2320

    Simu ya Kiganjani: +255 688639341

    Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovutii

Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.