• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mpwapwa District Council
Mpwapwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
        • Fedha
        • Biashara
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Mali asili
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Usafi na Mazingira
      • Utawala na Utumishi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Habari Mawasiliano na Tehama
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
    • Mamlaka
      • Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mpwapwa
      • Mamlaka ya Maji Mpwapwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashuri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa mbali mbali
    • Fomu za Maombi
    • Miongozo mbali mbali
    • Simulizi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video mbali mbali
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

CMT Yafanya Ufuatiliaji wa Ujenzi wa Kituo vya Afya Mtera, Baada ya Kulegalega.

Posted on: January 9th, 2021

Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa Dc.

Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa (CMT) ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndugu Paul M. Sweya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wamefanya ufuatiliaji wa Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mtera. Fedha za ujenzi wa Kituo cha Afya Mtera zilitokana na  wananchi wa Kijiji cha Mtera kumuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwajengea kituo cha Afya katika kijiji hicho wakati akitokea Iringa katika Siku ya Mei Mosi 2018. Mhe. Rais Magufuli aliridhia ombi la wananchi hao na ndipo aliagiza fedha zitolewe kwa ajili ya kujenga Kituo cha Afya cha Mtera. Fedha zilizotololewa ni Shilingi Milioni mia nne tu (Tsh 400,000,000/=).

Timu ya Menejimenti na Kamati ya Ujenzi wakiwa katika majumuisho baada ya kukagua majengo yote ya Kituo cha Afya Mtera.

Mnamo mwezi Aprili mwaka 2020 Kituo cha Afya cha Mtera kilianza kujengwa, majengo matano yalianza kujengwa ikiwemo Jengo la Maabara, Jengo la Upasuaji, jengo la mama na mtoto, jengo la Kuhifadhia maiti na Jengo la Mionzi (X-ray), ambapo kutokana na mkataba majengo yote matano yalitakiwa kukamilika mwezi Juni 2020 lakini mpaka sasa hayajakamilika.

Kutokana na kusuasua kwa ukamilishwaji wa Ujenzi wa Kituo cha Afya hicho, Timu ya menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imeamua kufanya ziara ya ufuatiliaji ili kubaini sabubu ya kucheleweshwa kwa ujenzi huo.

Katika ziara hiyo Timu hiyo ilibaini kuwa kuna upungufu wa vifaa vya ujenzi kama saruji, milango hakufungwa kwa kuwa haijakamilika kutengenezwa, madirisha kwa baadhi ya majengo hayajawekwa, baadhi ya majengo hayana vigae vya sakafuni (Tiles), mfumo wa maji taka haujakamilika, milango ya jengo la x-ray iondolewe kwakuwa imepinda na iwekwe mipya, madirisha mawili katika jengo la mama na mtoto yalikuwa hayana ubora na hayafanani na mengine kwa urembo (maua) uliowekwa, sinki la kunawia mikono halijawekwa katika ubora unaotakiwa, baadhi ya mafundi wameterekeza kazi.

Timu ya Menejimenti Ikikagua Ujenzi wa Majengo ya Kituo cha Afya cha Mtera.

Baada ya Ukaguzi wa kina Timu ya Menejimenti na Kamati za Usimamizi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Mtera walikaa kikao cha pamoja na ndio Timu ya Menejimenti iliagiza yafuatayo: 

1. Fundi Bahati Sanga aliyetoweka katika eneo la kituo kwa sababu ya kudai kuwa anauguliwa ajulishwe kwa barua kuwa akabidhi kazi ikiwa imekamilika ifikapo tarehe 20 Januari 2021.

2. Fundi wa milango na madirisha akamatwe na apelekwe polisi kuhojiwa na ajulishwe ifikapo tarehe 20 Januari 2021 kazi zote ziwe zimekamilika na hakutakuwa na muda wa nyongeza.

3. Mganga Mkuu na Mafundi Sanifu (Technicians) watatu wahamie Mtera na watashirikiana na kamati ya Usimamizi wa ujenzi kwa muda wote mpaka kituo kitakachokamilika ifikapo tarehe 20 Januari 2021.

4. Vifaa vyote vilivyokwisha vinunuliwe ili kazi ikamilike kwa wakati.

5. Mapungufu yote yaliyobainika yarekebishwe ikiwemo madirisha yabadilishwe, milango ibadilishwe, vigae vya sakafuni viwekwe, masinki ya kunawia mikono yarekebishwe. 

Fundi Aking'oa Dirisha lenye kiwango cha Chini na lenye urembo tofauti na mengine baada ya Kuamurishwa na Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya WiIaya ya Mpwapwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya, ameishukuru Timu ya Menejimenti kwa ziara yao yenye manufaa na kubaini mapungufu hayo, pia amehaidi kwa niaba ya kamati nzima kusimamia kwa dhati na kurekebisha mapungufu hayo ili kituo kikamilike ifikapo tarehe 20 Januari 2021.

Mwisho, Ndugu Sweya aliwashukuru wanakamati ya Usimamizi wa Ujenzi kwa Usimamizi mzuri hadi kufikia hapa japo kulikuwa na changamoto nyingi na hivyo kuwataka kuendelea kujitoa kusimamia Ujenzi wa Kituo hicho kwa kuwa wao ndio watakaonufaika pamoja na wananchi kwa ujumla.

Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usahili MpwapwaDC June 27, 2022
  • Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa May 2022 May 31, 2022
  • Tangazo la kuahirishwa kwa Usahili Halmashauri ya Mpwapwa June 22, 2022
  • Tangazo la Kuahirishwa kwa kikao cha Kamati ya Fedha uongozi na Mipango March 31, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mgao wa Pikipiki Kwa Watendaji wa Kata

    March 01, 2023
  • Mtokeo ya kidato cha nne yatangazwa

    January 29, 2023
  • Matokeo ya Mtihani Darasala nne na Kidato cha Pili 2022

    January 04, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Saba yatangazwa

    December 01, 2022
  • Tazama zote

Video

Video ya Mpango wa Uuzaji wa Viwanja Eneo la Mazae Block "E" katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa -2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
  • Muundo wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani
  • Ratiba ya Vikao vya Madiwani

Viunganishi Linganishi

  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Utumishi portal
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu Teknolojia na Sayansi
  • Sekretarieti ya Ajira

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mpwapwa - Dodoma, Tanzania

    Anwani: S.L.P 12

    Simu: 255 26 2320122/2320

    Simu ya Kiganjani: +255 688639341

    Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovutii

Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.