Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe.Dkt Sophia Mfaume Kizigo leo Agosti 12,2024 ameeanza ziara yake yakusikiliza kero za Wananchi na kuzitatua na kutembelea Miradi ya kimaendeleo inayoendelea kujengwa katika kata ya Ng’ambi,Chunyu na Mzae.
Katika Ziara yake hiyo iliyoanzia Kata ya Ng’ambi Mhe.Kizigo ametembele mradi wa ujenzi wa vyoo vya Zahanati ya Ng’ambi uligharimu kiasi cha Shillingi Million kumi na saba,na kukagua jengo la kuhifadhia dhana za Kilimo kama vile Matrekta,Power tiller,Mashine za kulima,kupanda na kuchakachulia nafaka na kufuatia na mkutano wa hadhara uliotoa fursa kwa Wananchi kutoa kero zao na Changamoto walizonazo katika kijiji chao,mkutano huo umetoa fursa kwa Mhe kuwapongeza Wananchi wa Ng’ambi kwa utunzaji mzuri wa miradi ya EBBAR.
Pia katika kata ya Chunyu ametembelea kambi ya mradi wa Barabara kutoka round ya bout ya kongwa Mpwapwa,Mpwapwa Kibakwe pamoja na kufanya mkutano na wananchi kusikiliza kero zao.
Halikadhalika amekagua mradi wa zahati ya Kisokwe pamoja na kufanya mkutano wa hadhara na Wananchi wa kijiji cha Idilo wa kata ya Mazae.
Mhe.Kizigo ametoa maagizo mbali mbali kwea viongozi wa kila kijiji kwa kuhakikisha wanafanya mikututano na wananchi wao na kuwajuza mapato na matumizi yanayotumika ndani yz vijiji vyao,pia kupimwa kwa matirio ya vifaa yaliyotumika katika ujenzi,mbali na hayo amewakumbusha Wananchi kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuchaguz viongozi wanaofaa.
"KERO YAKO WAJIBU WNGU"
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.