• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mpwapwa District Council
Mpwapwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
        • Fedha
        • Biashara
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Mali asili
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Usafi na Mazingira
      • Utawala na Utumishi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Habari Mawasiliano na Tehama
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
    • Mamlaka
      • Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mpwapwa
      • Mamlaka ya Maji Mpwapwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashuri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa mbali mbali
    • Fomu za Maombi
    • Miongozo mbali mbali
    • Simulizi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video mbali mbali
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

FUM Yatembelea Miradi

Posted on: November 2nd, 2018

(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Donath S. Nghwenzi akiwa na Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango pamoja pamoja na baadhi ya wataalam toka Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa leo amefanya ziara katika miradi sita yenye thamani ya Tshs.1,599,800,000.00. katika miradi hiyo, miradi mitatu ni ya sekta ya Elimu ambayo ni Shule ya Sekondari Pwaga imepata fedha Tsh. 66,600,000.00, Shule ya Sekondari Massa imepata fedha Tsh. 66,600.000.00 na Shule ya Sekondari Chipogoro imepata Tsh. 66,600,000.00,  Miradi mingine Mitatu ni ya sekta ya Afya ambayo ni Kituo cha Afya Pwaga imepata fedha Tsh. 500,000,000.00, kituo cha Afya Kibakwe imepata fedha Tsh. 400,000,000.00 na Kituo cha Afya Mima imepata fedha Tsh. 500,000,000.00. Fedha zote za ujenzi wa vituo vya afya ni fedha serikalini katika Mfuko Maalum wa Afya. Kwa ujumla vituo vyote vitatu vya afya vipo katika hatua ya umaliziaji.

Kwa upande wa sekta ya Elimu shule ya Sekondari Pwaga ilipewa fedha kiasi cha Tsh 66,600,000.00 zilizotolewa toka Mradi wa Lipa kutokana na Matokeo (P4R) kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 3 na matundu ya vyoo 6 ambapo ujenzi umekamilika na madarasa na vyoo  vinatumika. Katika fedha hiyo iliyotolewa, ni Tsh 56,615,500.00 na fedha iliyobaki Tsh 9,984,500 iliombewa idhini ili itumike katika ukarabati wa jengo utawala, ununuzi waviti 30 vya walimu, kuweka umeme katika nyumba za walimu, kukarabati vyoo vya zamani vya wanafunzi, kununua meza za walimu na kukarabati madarasa 10 ya zamani. 

Mhe. Nghwenzi amempongeza sana mkuu wa shule ya sekondari Pwaga kwa usimamizi mzuri wa fedha na miradi ya serikali na kwa kununua vifaa vya ujenzi kwa bei ya soko (bei halisi). Pia ametoa wito kwa wataalam wote wa Halmasahuri ya Wilaya ya Mpwapwa kusimamia miradi ya serikali vizuri na kwa ubora kama Mkuu wa Shule ya Sekondari Pwaga Ndug. Augustine Senya.

Mojapo ya darasa la shule ya sekondari Pwaga lilojengwa kwa fedha za P4R, jumla ni madarasa matatu yamekarabitiwa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Donath S. Nghwenzi (wanne kushoto) akiwa katika moja ya darasa lililojengwa kwa fedha za P4R akionyeshwa madawati na kukagua ujenzi uliofanyika.

Jengo la Choo cha matundu sita kilichojengwa kwa fedha za P4R katika shule ya sekondari ya Pwaga

Kwa upande wa sekta ya Afya, Kituo cha Afya Kibakwe kimepokea fedha Tsh 400,000,000.00 toka serikalini katika Mfumo Maalaum Wa Afya ambapo fedha hizo zimetumika kujenga jengo la wagonjwa wa nje (OPD) ndani yake kuna maabara na ofisi mbalimbali za madaktari, chumba cha upasuaji, wodi ya wazazi, wodi ya wanaume, wodi ya wanawake, nyumba ya mtumishi na jengo la kuhifadhia maiti. Mpaka sasa Majengo yote yapo katika hatu ya umaliziaji na matengenezo madogo madogo na ifikapo Novemba 30, 2018 kituo hiki cha Afya kitakuwa kimekamlika na kuanza kutumika.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Donath S. Nghwenzi amemuagiza mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ambaye ni Afisa utumishi na rasilimali watu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuwa asimamie ukamilishwaji wa Kituo hiki cha Afya na ifikapo tarehe 30 Novemba 2018 wananchi waweze kupata huduma iliyokusudiwa. Pia ameagiza kuwa ifikapo tarehe 30 Novemba 2018 vituo vyote vitatu maana Kituo cha Afya Mima, Kituo cha Afya Kibakwe, na Kituo cha Afya Pwaga viwe vimekamilika ili wananchi wapate huduma.

Jengo la upasuaji katika Kituo cha Afya Kibakwe

 Jengo la Wodi ya Akina Mama Kwa Ndani katika Kituo cha Afya Kibakwe

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Donath S. Nghwenzi (katikati) akielekea kwenye jengo la kuhifadhia Maiti katika Kituo cha Afya Kibakwe.Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) Kituo cha Afya Kibakwe

Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa.

Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usahili MpwapwaDC June 27, 2022
  • Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa May 2022 May 31, 2022
  • Tangazo la kuahirishwa kwa Usahili Halmashauri ya Mpwapwa June 22, 2022
  • Tangazo la Kuahirishwa kwa kikao cha Kamati ya Fedha uongozi na Mipango March 31, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mgao wa Pikipiki Kwa Watendaji wa Kata

    March 01, 2023
  • Mtokeo ya kidato cha nne yatangazwa

    January 29, 2023
  • Matokeo ya Mtihani Darasala nne na Kidato cha Pili 2022

    January 04, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Saba yatangazwa

    December 01, 2022
  • Tazama zote

Video

Video ya Mpango wa Uuzaji wa Viwanja Eneo la Mazae Block "E" katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa -2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
  • Muundo wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani
  • Ratiba ya Vikao vya Madiwani

Viunganishi Linganishi

  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Utumishi portal
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu Teknolojia na Sayansi
  • Sekretarieti ya Ajira

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mpwapwa - Dodoma, Tanzania

    Anwani: S.L.P 12

    Simu: 255 26 2320122/2320

    Simu ya Kiganjani: +255 688639341

    Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovutii

Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.