Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa Dc
Mkuregenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndugu. Paul M. Sweya ameamua kuchukua hatua ya kutengeneza madawati kwa kuwatumia mafundi wa ndani waliopo katika Idara ya Ujenzi. Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imenunua mbao na kuweza kutengeneza madawati arobaini (40) ya awali ambapo kila dawati moja linauwezo wa kukaa wanafunzi watatu (3), na kwa kuwa zoezi hili ni hili ni endelevu. Kwa ujumla katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuna shule nyingi hasa za msingi hazina madawati ya kutosha.
Madawati arobaini yakishushwa katika Shule ya Msingi Idilo
Pia Halmashauri imeomba kibali cha kukata miti na kuchana mbao, katika msitu mdogo wa kupandwa uliopo karibu na Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa ili kutengeneza madawati zaidi ili kunusuru wanafunzi wanakaa chini katika shule mbalimbali za Serikali hususan shule za msingi.
Vilevile Mkuregenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndugu Sweya, amemuagiza Kaimu Afisa Elimu Msingi Ndugu Alexander Kiowi afuatilie shule zote 120 za Msingi ili kupata idadi ya madawati mabovu yanayohitaji ukarabati ili waweze kukarabatiwa. Hii itasaidia kupunguza idadi ya wanafunzi wanaokaa chini.
Mafundi wakichana mbao zitakazotumika katika utengenezaji wa Madawati (Miti imevunwa katika msitu mdogo karibu na Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa)
Hata hivyo madawati hayo 40 ya awali yamepelekwa katika Shule ya Msingi Idilo iliyopo kata ya Mazae ambapo Darasa la kwanza, la pili na la tatu wanakaa chini, kwa kuwa zoezi hilo ni endelevu. Madawati yaliyopelekwa ni ya kukaa wanafunzi watatu kwa dawati moja.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Idilo wakiwa wamekaa katika madawati mara baada ya Shule yao kukabidhiwa matawati toka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
Mwisho, Ndugu Sweya ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia madawati ili kunusuru wanafunzi wanaokaa chini katika Shule za Msingi na baadae kuweza kupandisha kiwango cha ufaulu Wilayani Mpwapwa.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.