Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) chini ya kiongozi Mhe. Grace Peter Tendega leo imetembelea Halmasahuri ya Wilaya ya Mpwapwa. Katika ziara hiyo wajumbe wa kamati hiyo wametembelea na kukagua miradi ya Ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa Shule ya Msingi Vinghawe na ujenzi wa ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa. Kamati imebaini katika uwekaji wa silingibodi upande wa nyuma wa jengo haikuwekwa, hivyo kamati imemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndugu Mwanahamishi H. Ally kuhakikisha sehemu iliyobaki inawekwa silingibodi kwa wakati.
Kamati ya Bunge ikiongozwa na Mhe. Tendega (wa tano kulia waliosimama mbele) wakikagua moja ya darasa katika shule ya Msingi Vinghawe.
Aidha katika Ujenzi wa Ukumbi wa Halmashauri Kamati imebaini ujenzi kusimama kwa muda mrefu na Halmashauri kutenga bajeti kidogo katika umaliziaji wa ukumbi huu.Kamati imeagiza ndani ya miezi mitatu Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ihakikishe imeandika andiko na kuliwasilisha Wizara ya Fedha ili kuweza kupata fedha za kumalizia jengo hili.
Kamati ya Bunge ikikagua jengo la ukumbi wa Halmashauri
Mwisho Mwenyekiti wa Halamashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. George Fuime amewashukuru wajumbe wa kamati ya Bunge kwa kuitembelea Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa na kuahidi kuyasimamia yote yaliyoagizwa na kamati.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.