(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango leo imekagua baadhi ya miradi ya maendeleo wilayani Mpwapwa katika kata za Berege, Mpwapwa Mjini, Chunyu, na Mazae. Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa Mkataba na Bwaro katika Shule ya Sekondari Mazae kata ya Mazae, Ukaguzi wa Magari mabovu yaliyopaki katika yadi ya Idara ya Ujenzi, ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya Msingi Msagali kata ya Chunyu, na ujenzi wa maktaba moja, madarasa mawili na bwalo la chakula katika shule ya sekondari Berege katika kata ya Berege.
Ukaguzi huo wa miradi umeongozwa na Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. George Fuime pamoja na wajumbe wa Kamati ya Fedha na wataalam tako Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.
Katika Ukaguzi wa Magari sita mabovu ya Halmashauri yaliyopaki kwa muda mrefu katika yadi ya Ujenzi yamegundulika kuwa mengi ni mabovu sana, pia ni gharama kubwa kuyatengeneza na hivyo Kamati ya Fedha imependekeza kuwa ufanyika utaratibu magari haya yauzwe kwa sababu Halmashauri haina fedha ya kuweza kuyafufua. Pendekezo hilo la kuuza magari haya limejiri baada ya kukagua na kubaini ubovu wa magari hayo ambapo Halmashauri hayawezi kuyafufua kwa kuwa gharama yake ni kubwa.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango wakikagua magari mabovu katika yadi ya Ujenzi
Aidha wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango wamempongeza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msagali Ndugu. Medard Mgube Tuju kwa usimamizi mzuri wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa ufadhiri wa Mfuko wa Elimu Lipa kutookana na Matokeo (EP4R) ambapo amefanikiwa kukamilisha madarasa hayo kwa wakati na kufuata miongozo ya matumizi ya fedha zilizotolewa ambazo zilikuwa jumla ya Tsh. 25,000,000/= Kwa sasa madarasa hayo yapo tayati kwa matumizi ana kamati ya fedha imeshauri kuwa madarasa haya kwa kuwa yanaumeme na madirisha ya vioo ni bora wakasomea wanafunzi wa madarasa ya juu kama darasa la nne, tano, sita na saba kwa kuwa wanauelewa na wanaweza kutunza miundombino ya madarasa haya.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango wakisomewa taarifa ya Ujenzi wa Madarasa Mawili katika Shule ya Msingi Msagali
Ukaguzi wa Miradi umeendelea katika Shule ya Sekondari Berege ambapo kuna ujenzi wa Madasa mawili, maktaba moja na bwaro unaendelea. Japo katika maeneo mengi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa majengo kama haya yameshakamilika na mengine yapo katika hatu ya umaliziaji ila hapa katika shule ya Sekondari Berege ujenzi bado unasuasua sana. Kufuatia hali hiyo Kamati ya Fedha imekufanya kikao na kamati ya ujenzi, walimu, na mafundi kujua changamoto zilizopo ambapo Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ameeleza kuwashida kubwa ni kuwa fedha zilifungwa tangu tarehe 30/06/2018 wakati mwaka wa fedha ulipoisha. Pia Afisa Mipango wa Wilaya ya Mpwapwa Ndugu. Nackam Nchimbi ameeleza kuwa kwa sasa jitihada za kuingiza vifungu vya bakaa katika mfumo wa FFARS ili kuweza kusaidia fedha zilizobaki zilipwe na kazi hii iendelee vizuri na iishe kwa wakati.
Kutokana na maelezo ya matumaini ya Afisa Mipango wa Wilaya, kamati ya Fedha imeagiza kuwa ifikapo tarehe 25/09/2019 majengoo yote yanayoendelea kujengwa yawe yameisha.
Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango wakifanya kikao na kamati ya Ujenzi katika Shule ya Sekondari Berege ndani ya Bwaro linaloendelea kujengwa.
Mwisho Kamati ya Fedha imempongeza fundi Mkuu anayejenga jengo la Bwaro kuwa ni fundi stadi na mbunifu, hivyo amejenga vizuri kwa kuzingatia ramani na kunyoosha kuta vizuri.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.