• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mpwapwa District Council
Mpwapwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
        • Fedha
        • Biashara
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Mali asili
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Usafi na Mazingira
      • Utawala na Utumishi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Habari Mawasiliano na Tehama
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
    • Mamlaka
      • Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mpwapwa
      • Mamlaka ya Maji Mpwapwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashuri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa mbali mbali
    • Fomu za Maombi
    • Miongozo mbali mbali
    • Simulizi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video mbali mbali
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Kamati ya LISHE Wilaya Yajengewa Uwezo

Posted on: March 21st, 2019

(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)

 Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Mpwapwa Ndugu. Khamlo Njovu ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndugu Paul Sweya, amefungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Kamati ya Lishe ya Wilaya ya Mpwapwa katika Ukumbi wa Mamlaka ya Maji Mpwapwa. Katika mafunzo haya wadau mbalimbali wa LISHE Endelevu wamehudhuria kama vile Jukwaa la Utu wa Mtoto, Action Against Anger, Save the Children, Taasisi ya Chakula na lishe, Ofisi ya Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma, Diloitte, Wakuu wa Idara, Viongozi wa dini, taasisi binafsi zinazojihusisha na mashuala ya LISHE.

Madhumini ya mafunzo haya ni kuwapitisha wajumbe wa Kamati ya LISHE Wilaya katika Mpango Mkakati wa Wa Taifa ambao umetaja kila majukumu ya wadau wa LISHE toka ngazi ya Kitaifa, Wizara, Mikoa, Wilaya, Tarafa, Kata, Vijiji mpaka kwa jamii. Mpango Mkakati huo umeeleza masuala mengi ya lishe ikiwemo jinsi ya kuwashirikisha wadau wengine katika masuala ya lishe ambao ni muhimu. 

Wajumbe wa kamati ya LISHE Wilaya ya Mpwapwa pamoja na Wadau wa LISHE wakiwa katika Ukumbi wa Mamlaka ya Maji Mpwapwa wakifuatilia mafunzo ya LISHE

Aidha mtoa mada ameutambulisha Mpango Mkakati wa Taifa wenye agenda na shughuli mbalimbali kuanzia ngazi ya wizara hadi katika ngazi ya jamii. Pia ameongeza kuwa katika Mpango Mkakati kila mdau anategemea mdau mwingine, mfano: wadau wa kilimo wanawategemea wadau wa viwanda na sekta ya maji, hivyo double duty interaction ina maana kuwa katika masuala ya LISHE wadau mbalimbali wanapaswa kuhusishwa.

Pia Mpango mkakati umeainisha bayana namna ya kufanya ufuatiliaji na tathmini katika ukekelezaji wa shughuli za LISHE zilizofanywa na kuwashrikisha wadau mbalimbali wa lishe kama wazalishaji wa vyakula, vinywaji, na chumvi ili kuweza kuwahamasisha kuweka virutubisho muhimu katika bidhaa wanazozizalisha lengo likiwa ni kuiwezesha jamii kupata virutubisho hivyo kupitia bidhaa wanazozitengeneza na kuziuza kwa jamii. 

Vilevile kamati ya LISHE imefundishwa namna ya kufahamu Utapiamlo mkali ambao husababishwa na mtu kutopata chakula cha kutosha na kisichokuwa na virutubisho kama vitamini, madini chumvi, protein na virutubisho vingine.

Aidha Mpango Mkakati wa Taifa huu umefuata mabadiliko ya jamii kama kupata chakula bora, afya bora, ukosefu wa rasilimali, kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari, ini, figo na shinikizo la juu  la damu, hivyo tunatazamia kuwa watoto, wanawake, vijana na wanaume watakuwa na afya bora ya kuweza kufanyakazi na kuzalisha mali.

Wajumbe wa kamati ya LISHE Wilaya ya Mpwapwa pamoja na Wadau wa LISHE wakiwa katika Ukumbi wa Mamlaka ya Maji Mpwapwa wakifuatilia mafunzo ya LISHE

Mpango huu wa Mkakati wa Taifa umetaja matumizi ya vyoo bora na kutumia kanuni za afya vizuri ili kuepukana na kupata magnjwa ya mlipuko kama kipindupindu na hivyo wananchi kuwa na afya imara.

Mwisho wajumbe wa Kamati ya LISHE Wilaya wamegawiwa Tool Kit na Kitini cha Masuala ya LISHE kama vitendea kazi katika majukumu yao ya kila siku ya LISHE. Pia Mwenyekiti wa Mafunzo hayo ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji amewashukuru wote waliotoa mafunzo  haya na ameaidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa niaba ya wajumbe wote wa kamati ya LISHE Wilaya ya Mpwapwa. 


Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usahili MpwapwaDC June 27, 2022
  • Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa May 2022 May 31, 2022
  • Tangazo la kuahirishwa kwa Usahili Halmashauri ya Mpwapwa June 22, 2022
  • Tangazo la Kuahirishwa kwa kikao cha Kamati ya Fedha uongozi na Mipango March 31, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mgao wa Pikipiki Kwa Watendaji wa Kata

    March 01, 2023
  • Mtokeo ya kidato cha nne yatangazwa

    January 29, 2023
  • Matokeo ya Mtihani Darasala nne na Kidato cha Pili 2022

    January 04, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Saba yatangazwa

    December 01, 2022
  • Tazama zote

Video

Video ya Mpango wa Uuzaji wa Viwanja Eneo la Mazae Block "E" katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa -2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
  • Muundo wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani
  • Ratiba ya Vikao vya Madiwani

Viunganishi Linganishi

  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Utumishi portal
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu Teknolojia na Sayansi
  • Sekretarieti ya Ajira

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mpwapwa - Dodoma, Tanzania

    Anwani: S.L.P 12

    Simu: 255 26 2320122/2320

    Simu ya Kiganjani: +255 688639341

    Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovutii

Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.