(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa).
Kamati ya Lishe ya Wilaya ya Mpwapwa imefanja kikao cha Robo ya NNe kwa mwaka wa fedha 2018/2019, kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa na kuhudhuriwa na Wajumbe wa kamati hiyo.
Akifungua kikao hicho Ndugu. Khamlo Njovu Afisa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, amewaongoza wajumbe wa Lishe katika kupitia na kuchambua kwa kina Taarifa ya Robo ya Nne 2018/2019 ya Utekelezaji wa Shughuli za Lishe zilizofanywa na idara mtambuka katika masuala ya lishe. Idara hizo ni kama vile Afya, Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika, Ufugaji na Uvuvi, na Usafi na Mazingira.
Mkaratibu wa Lishe Wilaya ya Mpwapwa Ndugu Renatus Komba (kusho mbele) akiwasilisha mada za Lishe kwa Kamati ya Lishe ya Wilaya ya Mpwapwa
Wajumbe wa Kamati ya Lishe ya Wilaya ya Mpwapwa Wakiwa katika Ukumbi wa Halmashauri kwa ajili ya Kupanga na kujadili mikakati na taarifa za Lishe ya Robo ya Nne ya Mwaka wa Fedha 2018/2019
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.