(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Jopo la Madaktri Bingwa kutoka katika Hospitali mbalimbali maarufu ikiwemo Muhimbili, Benjamini Mkapa - Dodoma, Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na CCBRT leo wameanza kazi rasmi ya matibabu kwa wagonjwa wenye magonjwa yanayohitaji utaalam wa hali ya juu katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa. Madaktari hao wamekuja kutokana na zoezi la kuwepo kwa Kliniki Tembezi ambayo hufanyika kila mwaka ambapo madaktari bingwa kutoka katika Hospitali Maarufu huja Mpwapwa kushirikiana na wenzao ili kuweza kutibu kwa pamoja magojwa yanayohitaji utaalam wa hali ya juu. Zoezi kubwa leo ni kuwasajili wagonjwa na wachache wamefanikiwa kuwaona madaktari na kupatiwa matibabu.
Hili ni moja ya basi kati ya mabasi matatu yaliyowasafirisha madaktari bingwa kuja wilayani Mpwapwa kwa ajili ya kutoa huduma katika Kliniki Tembezi
Madaktari bingwa wakiwa katika kikao cha pamoja na wenyeji (madaktari wa wilaya) wakijadili mikakati ya kazi
Wahudumu wakiwa katika Zoezi la uandikishaji wa wagonjwa katika viwanja vya Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa
Huyu ni mhudumu wa Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa aliyevaa tangazo la NIULIZE MIMI, kazi yake ni kuwaelekeza wagonjwa wageni mahali anapohitaji kwenda ili kupata huduma
Vibanda hivi ni kwa ajili ya uandikishaji wa wagonjwa ili wakaonane na madaktari bingwa
Hili ni jengo la Maabara ya Kisasa yenye vifaa vya kisasa na wataalam waliobobea katika taaluma ya Maabara katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.