Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge amefanya ziara ya kukagua mradi wa maji katika kijiji cha Bumila kata ya Lupeta Wilayani Mpwapwa. Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa amepata fursa ya kukagua ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 100,000 linalotarajia kuhudumia wananchi 2204 kwa mujibu wa makadirio ya mwaka 2019. Mradi huo umejengwa na Kampuni ya Advanced Engineering Company ya Dar es salaam kwa mkataba namba LGA 023/2016-2017 ambao ulisainiwa tarehe 16/11/2017 ulitakiwa kumamilika tarehe 10/05/2018 na unafadhiliwa na Mradi wa Program ya Maji na usafi wa Mazingira Vijijini (NRWSSP) wenye thamani ya Tsh 637,957,268.
Mpaka sasa mkandarasi amelipwa Tsh 303,879,609.99 na anadai Tsh 334,077,654 bado hajalipwa kwa sababu fedha zilichewa na hivyo kuna baadhi ya kazi hazijakamilika.
Akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo wa maji Bw. Ngwembele (Technician) kwa niaba ya Mhandisi Christina Msengi, kuwa ujenzi umekalika kwa kazi ya ujenzi wa jengo la COWSO, tanki, vituo 14 vya kuchota maji, nyumba ya mashine ya kusukuma maji, mlambo wa kunyeshea mifugo na mabomba yamelazwa, ila bado pampu na miundombinu ya umeme haijakamilika, hivyo mkandarasi atakamilisha.
Kazi zilizobaki ni kufunga mota, pampu na mfumo wa umeme, kazi hizo hajamalizika kwa wakati kutokana na kuchelewa kwa fedha, mara nyingi baada ya kuomba fedha huwa zinachukua muda wa miezi sita hadi kutolewa.
Baada ya kumalisha kusomewa taarifa fupi ya mradi Mkuu wa Mkoa alitoa kasoro za tanki la maji ambalo kutokana na taarifa inaonyesha kuwa limekamilika. Kasoro hiyo ni kuwa tanki hilo lina nyufa kwa chini na hivyo mkandarasi asilipwe mpaka azibe ufa huo. Dkt. Mahenge amesema "nimekagua nikiwa na Mkuu wa Wilaya, Mhandisi wa Maji wa Wilaya, mhandisi wa Tanroads na Mhandisi wa Maji mkoa tumeona tanki limepasuka chini kwa ndani na hivyo mkandarasi asilipwe fedha za tanki mpaka azibe nyufa hizo. Hii imetokana na kutomwagilia maji tu. Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa nisaidie kusimamia hili, huyu Mkandarasi asilipwe mpaka akamilishe kazi ya kuziba nyufa."
Mkuu wa Mkoa ameahidi kuwa atawasiliana na Waziri wa Maji ili fedha zikiombwa ziweze kutolewa kwa wakati ili miradi ya maji iweze kukamilika kwa wakati.
Pia Mkuu wa Mkoa amewataka wahandisi wa maji wa wilaya kusimamia miradi ya maji kwa ukamilifu ili kuweza kuwa na miradi inayodumu na endelevu. Akitolea mfano wa tanki hili la Bumila kupasuka chini ni kwa sababu ya kutosimamia vizuri kwa kuwa kosa lililofanyika hapa ni kutokumwagilia maji ya kutosha ndio maana nyufa zimetokea.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.