• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mpwapwa District Council
Mpwapwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
        • Fedha
        • Biashara
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Mali asili
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Usafi na Mazingira
      • Utawala na Utumishi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Habari Mawasiliano na Tehama
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
    • Mamlaka
      • Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mpwapwa
      • Mamlaka ya Maji Mpwapwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashuri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa mbali mbali
    • Fomu za Maombi
    • Miongozo mbali mbali
    • Simulizi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video mbali mbali
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Mkuu wa Wilaya Afungua Kikao Kazi cha Lishe

Posted on: November 25th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri leo amefungua kikao kazi cha maandalizi ya awali ya ujumuishwaji wa afua za lishe katika mipango na bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2019/20. Mafunzo yaliyotolewa katika kikao hiki yamehudhuriwa na wakuu wa idara na taasisi za wilaya ya Mpwapwa, Wataalam wa Lishe toka OR - TAMISEMIna Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma, Wadau toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, na Wadau toka shirika la ACTION AGAINST HUNGER. Mafunzo haya yametolewa na kuwezeshwa na Serikali kupitia shirika la ACTION AGAINST HUNGER ili kufikia hatua muhimu katika uboreshaji wa shughuli za lishe Wilayani Mpwapwa. 

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri (watatu kushoto) akiwa  na wakuu wa idara, taasisi na wataalam wa lishe toka Mkoani Dodoma, OR TAMISEMI na Wizara ya Afya Nje ya Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mara baada ya kufungua Kikao kazi cha Kamati ya Lishe Wilaya.

Mhe. Shekimweri amesema, "Takwimu za 30/06/2018 katika zoezi la Upimaji wa Hali ya Lishe, utoaji wa dawa za minyoo na matone ya Vitamin A zimebaini kuwa utapiamlo bado ni tatizo kubwa linaloathiri watoto walio na umri chini ya miaka mitano hapa Wilayani Mpwapwa. Kwa mujibu wa takwimu; Udumavu ni asilimia 37, Uzito pungufu ni asilimia 12,Wakondefu ni asilimia 1. Hali hii ni mbaya na inahitaji nguvu kubwa ielekezwe kupunguza tatizo la utapiamlo kwa watoto wetu ambao ndio nguvu kazi ya taifa la kesho".Wajumbe wa Kikao kazi cha Kamati ya Lishe Wilaya wakisiliza kwa makini maelekezo ya mafunzo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa 

Mkuu wa Wilaya Mhe. Shekimweri katika hotuba yake amesema,  ikumbukwe kuwa;  mnamo tarehe 19/12/2017, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa niaba ya Makamu wa Rais alisaini Mkataba wa utekelezaji afua za lishe na Wakuu wa Mikoa yote nchini. Mkataba wenye lengo la kuchochea utekelewa shughuli za lishe kwa kasi hapa nchini utadumu kwa muda wa miaka minne (01 Januari, 2018 hadi Juni 30, 2021; na una viashiria kumi (10) ambavyo wakuu wa Mikoa wanapimwa majukumu kila baada ya miezi 6. Hivyo, natoa rai kwa watendaji wa ngazi zote na haswa kamati za lishe kutenga fedha kwenye mipango na bajeti kufuatana na miongozo yaani Tsh. 1000 kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano. Fedha hizi zitengwe kutoka kwenye vyanzo vinavyooaminika na usimamizi wa utekelezaji wa kila kiashiria uimarishwe zaidi. Ni matarajio yangu kuwa kila robo nipata taarifa ya utekelezaji na nataka nione matokeo yenye tija.

Sambamba na hilo Mkuu wa Wilaya ameagiza kuwa taarifa ya utekelezaji wa lishe ya kila robo mwaka iwasilishwe ofisini kwake na iwekwe katika tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, katika ziara zake Afisa Lishe na Afisa TEHAMA waambatane pamoja kwa ajili ya kutoa elimu ya lishe wa wananchi pamoja na kuzichukua taarifa hizo na kuziweka katika tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

Afisa LISHE wa Wilaya ya Mpwapwa akiwasilisha shughuli za lishe zilizotekelezwa kwa Wajumbe wa Kikao kazi cha Kamati ya Lishe Wilaya katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa 

Kamati ya Lishe ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imeazimia yafuatayo:-

1. Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa iendelee kutenga na kutoa fedha Tsh 1,000/= kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka 5.

2. Afisa lishe wa wilaya apewe siku ya kutoa semina yalishe katika kila vikao vya kisheria vya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa katika ngazi zote.

3. Lishe iwe ni agenda ya kudumu katika ngazi zote za kuanzia kijiji, kata, tarafa hadi wilaya, pia taarifa za Lishe ziingizwe katika kamati za kudumu za Halmashauri kwa ajili ya

    kuzisimamia na kutolea maamuzi wa mambo mbalimbali yanayohusu lishe.

4. Afisa lishe aandae mpango kazi wenye kutoa elimu, kutambulisha tatizo, kutoa njia ya kutatua na kufuatilia utekelezaji wake.

Kwa taarifa zaidi pakua nyaraka hizi:

Hotuba ya Mkuu wa Wilaya katika Kamati ya Lishe Wilaya ya Mpwapwa.pdf

Mada ya Lishe iliyowasilishwa na Afisa Lishe Wilaya ya Mpwapwa.pdf

Hali halisi ya Lishe.ppt

MKATABA LISHE.ppt

Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa.

Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usahili MpwapwaDC June 27, 2022
  • Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa May 2022 May 31, 2022
  • Tangazo la kuahirishwa kwa Usahili Halmashauri ya Mpwapwa June 22, 2022
  • Tangazo la Kuahirishwa kwa kikao cha Kamati ya Fedha uongozi na Mipango March 31, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mgao wa Pikipiki Kwa Watendaji wa Kata

    March 01, 2023
  • Mtokeo ya kidato cha nne yatangazwa

    January 29, 2023
  • Matokeo ya Mtihani Darasala nne na Kidato cha Pili 2022

    January 04, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Saba yatangazwa

    December 01, 2022
  • Tazama zote

Video

Video ya Mpango wa Uuzaji wa Viwanja Eneo la Mazae Block "E" katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa -2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
  • Muundo wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani
  • Ratiba ya Vikao vya Madiwani

Viunganishi Linganishi

  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Utumishi portal
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu Teknolojia na Sayansi
  • Sekretarieti ya Ajira

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mpwapwa - Dodoma, Tanzania

    Anwani: S.L.P 12

    Simu: 255 26 2320122/2320

    Simu ya Kiganjani: +255 688639341

    Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovutii

Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.