• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mpwapwa District Council
Mpwapwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
        • Fedha
        • Biashara
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Mali asili
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Usafi na Mazingira
      • Utawala na Utumishi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Habari Mawasiliano na Tehama
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
    • Mamlaka
      • Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mpwapwa
      • Mamlaka ya Maji Mpwapwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashuri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa mbali mbali
    • Fomu za Maombi
    • Miongozo mbali mbali
    • Simulizi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video mbali mbali
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Mkuu wa Wilaya Afungua Mafunzo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi

Posted on: May 25th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri leo amefungua mafunzo ya saratani ya malngo wa kizazi katika Ukumbi Mkubwa wa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa.  Mafunzo hayo ni ya siku moja na yametolewa na wataalam toka Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa wakiongozwa na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt. Said Mawji ambao walipatiwa mafunzo toka Wzara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. George Fuime, Wakuu wa idara wa Halmashuri ya Wilaya ya Mpwapwa, wakuu wa taasisi, wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama, maafisa tarafa na viongozi wa dini toka Wilaya ya Mpwapwa.

Katika hotuba yake Mkuu wa Wilaya amesema " Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau wa chanjo wametuambia itaazisha chanjo mpya ya kuwakinga na ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 kuanzia mwezi April, 2018 nchi nzima. Serikali imeamua kuanza kutoa chanjo hii kwasababu saratani ya mlango wa kizazi ndiyo inayoongoza kwa kuua wanawake wengi ukilinganisha na saratani nyingine hapa Tanzania."

Mhe. Jabir Shekimweri (Katikati) Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa akihutubia wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Saratani ya Mlango wa kizazi wilayani Mpwapwa (Picha Na: Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA, Mpwapwa)

Pia ametaja visababishi vichache vya saratani hiyo ni pamoja na kuanza kujamiana katika umri mdogo,kuwa na wapenzi wengi,kuwa na ndoa za matala,kuzaa watoto wengi, na vutaji wa sigara. Vilevile  Mhe. Kimweri ameorodhesha baadhi ya dalili za salatani ya mlango wa kizazi kama vile kutokwa damu ya hedhi bila mpangilio, kutokwa damu baada ya kujamiiana,maumivu ya mgongo, miguu na/au kiuno, kuchoka, kupungua uzito, kupungukiwa au kokosa hamu ya kula,kutokwa uchafu wa rangi ya kahawia au wenye
 damu kwenye uke,maumivu ya miguu au kuvimba. Dalili mbaya zaidi zinazoweza kujitokeza ni pamoja na kuishiwa damu, figo kushindwa kufanya kazi, kupatwa na fistula, na uvimbe wa tezi.

Mhe. George Fuime (aliyesimama) Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa akiipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli  kwa kujali afya za wananchi wake na kugharimia chanjo hii. Mhe. Fuime  amesema hayo wakati wa kufunga mafunzo ya chanjo ya Saratani ya Mlango wa kizazi wilayani Mpwapwa (Picha Na: Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA, Mpwapwa)

Pia amewaomba wadau wote walihudhuria mafunzo haya wasaidie kupeleka ujumbe huu wa kuanzishwa kwa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa mabinti wa miaka 14 ili waweze kukingwa na madhara makubwa yanayoweza kuwapata hapo baadae ya kuugua kwa maumivu makali sana na hatimaye kifo. Wengi wetu tumetembelea Ocean Road na kuona
 jinsi jamaa zetu wanavyopata mateso makali.

Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa umakini  mafunzo ya saratani ya mlango wa kizazi Wilaya ya Mpwapwa  (Picha Na: Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA, Mpwapwa)

Mwisho amewataka wanchi wote kujitokeze kwa wingi katika kuzungumzia chanjo hiyo katika hali chanya na kuwaondoa wananchi wote wasiwasi kuwa chanyo ni salama na haina madhara.

Dkt. Said Mawji (aliyesimama), Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa akitoa mafunzo ya saratani ya mlango wa kizazi na kuelezea chanjo ya saratani hiyo.

Kwa habari zaidi pakua nyaraka hizi hapa chini:

HOTUBA-MKUU WA WILAYA YA MPWAPWA JUU YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI.pdf

MIKAKATI WA KIMKOA KUHUSU UZINDUZI WA CHANJO [Compatibility Mode].pdf

Saratani ya mlango wa kizazi.pdf

HALI HALISI YA UPIMAJI MLANGO WA KIZAZI [Compatibility Mode].pdf

Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usahili MpwapwaDC June 27, 2022
  • Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa May 2022 May 31, 2022
  • Tangazo la kuahirishwa kwa Usahili Halmashauri ya Mpwapwa June 22, 2022
  • Tangazo la Kuahirishwa kwa kikao cha Kamati ya Fedha uongozi na Mipango March 31, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mgao wa Pikipiki Kwa Watendaji wa Kata

    March 01, 2023
  • Mtokeo ya kidato cha nne yatangazwa

    January 29, 2023
  • Matokeo ya Mtihani Darasala nne na Kidato cha Pili 2022

    January 04, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Saba yatangazwa

    December 01, 2022
  • Tazama zote

Video

Video ya Mpango wa Uuzaji wa Viwanja Eneo la Mazae Block "E" katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa -2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
  • Muundo wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani
  • Ratiba ya Vikao vya Madiwani

Viunganishi Linganishi

  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Utumishi portal
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu Teknolojia na Sayansi
  • Sekretarieti ya Ajira

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mpwapwa - Dodoma, Tanzania

    Anwani: S.L.P 12

    Simu: 255 26 2320122/2320

    Simu ya Kiganjani: +255 688639341

    Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovutii

Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.