(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabari Shekimweri leo amekabidhi jezi 11 kwa Timu ya Mipra wa Miguu ya Miami iliyopo katika kata ya Kibakwe. Mwishino mwa mwaka 2018 Timu hiyo ya Miami ya Kata ya Kibakwe ilituma ombi la kusaidiwa vifaa vya michezo ikiwemo jezi kwa Mkuu wa Wilaya. Mkuu wa Wilaya kwa upande wake ameamua kutoa jezi kumi na moja kwa timu hiyo. Jezi hizo amekabidhiwa kapteni wa timu hiyo Ndug. Sauli Malamla.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri (katikati) akikabidhi jezi katika Timu ya Mpira wa miguu Miami ya kata Kibakwe
Mkuu wa Wilaya amesema anania kubwa ya kuinua michezo katika Wilaya ya Mpwapwa na ataendelea kutoa vifaa vya michezo pale atakapo jaliwa kupata fedha za kununua vifaa hivyo.
Pia Mkuu wa Wilaya amesisitiza kuwa vijana wanapaswa kuwekeza katika vipaji vyao hasa michezo kwa kuwa michezo ni ajira na afya kwa mwili wa binadamu.
Ameongeza kuwa jezi hizo zitunzwe na zitumike kwa ajili ya michezo tu na sio kutumika kama nguo za kushindia, kwa maana baada ya mchezo kuisha zikusanywe,
zifuliwe na kuhifadhiwa.
Kwa upande wake Kapteni wa Timu ya Miami Kibakwe amemshukuru sana Mkuu wa Wilaya kwa msaada huo na kumuomba asichoke kupokea maombi yao ya vifaa
vya michezo pamoja na kuahidi kuzitunza jezi hizo.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.