• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mpwapwa District Council
Mpwapwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
        • Fedha
        • Biashara
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Mali asili
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Usafi na Mazingira
      • Utawala na Utumishi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Habari Mawasiliano na Tehama
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
    • Mamlaka
      • Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mpwapwa
      • Mamlaka ya Maji Mpwapwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashuri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa mbali mbali
    • Fomu za Maombi
    • Miongozo mbali mbali
    • Simulizi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video mbali mbali
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Mkuu wa Wilaya Asikiliza Changamoto za Wazee wa Mpwapwa

Posted on: December 3rd, 2019

(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri leo amefanya mkutano na Wazee wa Mji wa Mpwapwa ili kuwafahamisha wazee hao miradi inayoendelea katika Wilaya ya Mpwapwa na kusiliza changamoto zao. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa wa Mkuu wa Wilaya na kuhudhuriwa na; Katibu tawala wa Wilaya ya Mpwapwa, Wataalam mbalimbali na wazee.  

Wazee hao wana Umoja wao unaoongozwa na Mwenyekiti wao, Mzee Gabriel Mnyawami ambaye amesoma taarifa ya wazee wa Mpwapwa kwa niaba ya wazee wote mbele ya Mkuu wa Wilaya. Katika taarifa hiyo imeeleza chanagmoto na maombi kama yafuatayo:- 

1. Huduma ya afya zisizoridhisha kwa wazee na wapatapo huduma, dawa zote huambiwa wakanunue. Pia wameomba zahanati ya Kijiji cha Mbori ipandishwe hadhi na kuwa kituo cha             afya.

2. Katika kilimo kuwe na zao la biashara.

3. Wameomba waanzishiwe mfuko wa Fedha za Mikopo (Revolving fund) ambapo wanaweza kukopa kwa riba nafuu ili kuweza kuendesha shughuli zao.

4. Wameomba kupata taarifa ya  muendelezo wa Mamlaka ya Mji Mdogo  Mpwapwa, barabara ya lami, gari la zima moto na gari la maji taka.

5. Wameomba kuanzishwe Maktaba ya Wilaya, na taarifa ya upugufu wa vyumba vya madarasa na madawati.

6.  Wameomba ufafanuzi kwanini Maji hayatoshi  na yamekuwa ya shida katika mji wa mpwapwa.

7. Wameomba ufafanuzi kwa nini mradi wa ukumbi wa halmashauri bado ni kiporo.

8. Wameomba Ulinzi na usalama uimarishwe kwa kuwa kuna matapeli wengi katika Mji wa Mpwapwa kwa sasa; mfano eneo la Benki wazee huwa wanatapeliwa.

9. Wamemba ufafanuzi na suluhisho kwa nini TANESCO wanachelewesha kuweka umeme hata baada ya kulipia gharama zote?

Baada ya mada hizo kuwasilishwa, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Shekimweri ameanza na kufafanua jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano inayongozwa na Rais Mhe. Dkt. John P. Magufuli katika kuleta maendeleo ya Mpwapwa na Nchi kwa ujumla. Mhe. Shekimweri ameeleza kuwa Serikali inafanya ujenzi wa reli ya treni iendayokasi, barabara zinazounganisha Mikoa na Wilaya, ununuzi wa ndege mpya nane na nyingine mbili zipo hatua ya Ujenzi na kujenga bwawa kubwa la umeme mkoani Morogoro ambapo vyote hivyo vitasaidia katika kukuza uchumi wa Nchi yetu hivyo tuunge mkono jitihada hizo.

Wazee wa Mpwapwa wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa katika kikao kilichofanyika kati ya Wazee hao na Mkuu wa Wilaya (wa pili kusho ni: Mzee Mnyawami Mwenyeikti wa Umoja wa Wazee wa Mpwapwa)

Aidha katika Masuala ya Elimu, Mkuu wa Wilaya ameleeza kuwa;  Katika Elimu Serikali imetoa shilingi Milioni miatatu kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maboma katika shule mbalimbali ambayo yamemalizika na yanatumika kwa sasa. Pia katika upanuzi wa Chuo cha Ualimu cha mpwapwa Serikali imetoa shilingi bilioni 2.8 na itajenga Maktaba kubwa ya kisasa ambapo maktaba hiyo itatumika kwa utaratibu utakaopangwa ili kunufaisha watu wote. Vile vile Serikali imejenga Maktaba na Mabwaro ya kisasa katika shule za Sekondari zenye kidato cha tano na sita za  Kibakwe, Berege, Mazae na Mpwapwa ili watoto wetu waendelee kupata elimu bora.

Pia katika Afya Mhe. Shekimweri amesema kuwa; Kwa ujumla huduma za afya zimeimarika, changamoto zilizopo ni za kibinadamu kama kufanya kazi kwa mazoea na maadili mabovu hivyo wazee wangu tusaidiane kuwaongoza vijana wetu kuwa waadilifu, kuwajengea uwezo na kuwakemea na wasipojirekebisha watachukuliwa hatua. Kupitia fursa hii namuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya kuwa Orodha ya dawa kwa ngazi zote zibandikwe ili watu waweze kuona ni dawa zipi zinapatikana. Pia, tumepoke shilingi bilioni 1 na milioni 400 kwa ajili ya  ujenzi wa vituo vya afya vya Mima, Kibakwe na Pwaga. Hata hivyo katika kipindi hiki cha miaka minne tumepokea gari la wagonjwa (ambulance) mpya ya kituo cha Rudi, pia tumepewa shilingi Milioni 96 kwa ajili ya kukamilisha vituo vya afya. Vilevile Wilaya yetu ina changamoto ya Utapiamlo mkali ambapo tumejengewa jengo kwa ajili ya huduma za kuaanda lishe bora.

Pia Mkuu wa Wilaya ameeleza masuala ya kilimo kuwa; nawaomba wazee wangu tuendelee kuhimizana kulima kwa juhudi na kuondoka kabisa na dhana ya chakula cha msaada kwa kuwa hakipo kabisa, msimu wa kilimo hakuna watu kucheza pool table wafanye kazi na kulima mazao ya chakula na biashara  kama  korosho ili kuinua kipato cha familia na Halmashauri. ..

Wazee wa Mpwapwa wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa katika kikao kilichofanyika kati ya Wazee hao na Mkuu wa Wilaya 

Akiendelea kueleza Mkuu wa Wilaya amesema kuwa; katika wilaya ya Mpwapwa kuna barabara yenye urefu wa KM 1023 ambayo ipo chini ya TARURA na barabara yenye urefu wa KM 316 inasimamiwa na TANROADS. Katika miaka minne ya Serikali ya awamu ya tano kuna barabara nyingi zimejengwa kama Kidenge - Lufu ambayo tangu tupate uhuru hawajawahi kuwa na barabara ya Kizi - Mbuga hadi Lumuma.  Pia kuna barabara ya lami katika eneo la Mpwapwa Mjini yenye urefu wa KM 2.5 ambapo ujenzi unaendelea na ujenzi huo wa barabara za lami hapa mjini utazingatia pia uwekaji wa taa barabarani.

Aidha, katika masuala ya upatikanaji wa maji Mkuu wa Wilaya amekiri kuwa; Ni kweli mji wa Mpwapwa una uhaba wa maji, na katika ujio wa waziri wa maji Mpwapwa tulimueleza kuwa tunahitaji chanzo kipya cha maji. Pia serikali ilitoa shilingi bilioni 4.7 kwa miradi 10 ya maji ambayo ipo 90% ya umaliziaji na pindi itakapo kamilika uhaba wa maji kwa wilaya ya Mpwapwa utapungua.

Mkuu wa Wilaya pia amezungumzia masuala ya umeme, ambapo ameeleza kuwa; kwa maelezo ya waziri wa nishati kuwa mbunge wa Kibake Mhe. George Simbachawene alitusaidia sana kuviingiza vijiji vyote vya Mpwapwa katika mpango wa kuwekewa umeme. Hadi kufikia 2021 vijiji vyote vya Mpwapwa na vitongoji vyake vitakuwa na umeme wa mradi wa REA unaoendelea. Hata hivyo amewahakikishia wazee kuwa wananchi wote ambao wamecheleweshwa kuunganishiwa umeme baada ya kulipia wawasilishe orodha ya majina yao na mahali wanapoishi ili afanye mawasiliano na meneja wa TANESCO ili waweze kupata huduma hiyo.

Wazee wa Mpwapwa wamemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa majibu mazuri ya kutatua changamoto zao na ufafanuzi mzuri alioutoa katika kikao hicho. Pia wamemuomba Mkuu wa Wilaya kuwa asichoke kuwasikiliza maana wazee wanachangamoto nyingi na wa kuzitatua ni yeye.

Akifunga kikao hicho Mkuu wa Wilaya amewashukuru wazee kwa umoja wao na kukusanyika hapo ili kusikiliza mambo mbalimbali yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano. Pia amewapongeza wazee kwa kuwasilisha changamoto zenye tija kwa Wilaya yetu na ameahidi kuzitatua kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa miradi husika kama maji, barabara, afya, kilimo, elimu na umeme.



Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usahili MpwapwaDC June 27, 2022
  • Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa May 2022 May 31, 2022
  • Tangazo la kuahirishwa kwa Usahili Halmashauri ya Mpwapwa June 22, 2022
  • Tangazo la Kuahirishwa kwa kikao cha Kamati ya Fedha uongozi na Mipango March 31, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mgao wa Pikipiki Kwa Watendaji wa Kata

    March 01, 2023
  • Mtokeo ya kidato cha nne yatangazwa

    January 29, 2023
  • Matokeo ya Mtihani Darasala nne na Kidato cha Pili 2022

    January 04, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Saba yatangazwa

    December 01, 2022
  • Tazama zote

Video

Video ya Mpango wa Uuzaji wa Viwanja Eneo la Mazae Block "E" katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa -2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
  • Muundo wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani
  • Ratiba ya Vikao vya Madiwani

Viunganishi Linganishi

  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Utumishi portal
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu Teknolojia na Sayansi
  • Sekretarieti ya Ajira

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mpwapwa - Dodoma, Tanzania

    Anwani: S.L.P 12

    Simu: 255 26 2320122/2320

    Simu ya Kiganjani: +255 688639341

    Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovutii

Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.