• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mpwapwa District Council
Mpwapwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
        • Fedha
        • Biashara
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Mali asili
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Usafi na Mazingira
      • Utawala na Utumishi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Habari Mawasiliano na Tehama
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
    • Mamlaka
      • Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mpwapwa
      • Mamlaka ya Maji Mpwapwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashuri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa mbali mbali
    • Fomu za Maombi
    • Miongozo mbali mbali
    • Simulizi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video mbali mbali
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Mpwapwa Kujengwa Stesheni ya Treni ya Mwendokasi, Bw. Masanja K. Kadogosa Anena.

Posted on: July 4th, 2019

(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge amefanya ziara katika kata ya Gulwe Wilayani Mpwapwa ambako Reli ya Treni ya Mwendokasi (SGR) inaendelea na ujenzi. Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa akiwa na viongozi wa mkoa na wa wilaya ya Mpwapwa amefanya mkutano na wafanyakazi na wasimamizi wa mradi huo wa SGR katika eneo la Gulwe. Katika Mkutano huo Mkuu wa Mkoa ameelezwa kuwa Ujenzi wa Reli ya Treni ya Mwendokasi (SGR) unaendelea vizuri na kasi yake inaridhisha na hivyo kwa kipande cha kutoka Morogoro hadi Makutupora chenye urefu wa 376.5KM kitakamilika tarehe 25 Septemba 2021 kama makataba unavyosema.

Katika taarifa ya SGR iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC Bw. Masanja K. Kadogosa, imeelezwa kuwa kutoka Morogoro hadi Makutupora kutajengwa stesheni 8, kati ya hizo kubwa zitakuwa 2 na 6 zitakuwa stesheni za kati. Stesheni kubwa zitajengwa katika maeneo ya Kilosa Mjini na Dodoma  eneo la Kikuyu Kusini.  Stesheni za kati zitajengwa maeneo ya Mkata, Kidete, Gulwe (Mpwapwa), Igandu, Bahi na Makutupora. Katika Wilaya ya Mpwapwa stesheni itajengwa eneo la Gulwe ambapo kwa sasa ujenzi unaendelea.

Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi wa Mpwapwa kuchangamkia fursa zinazoletwa na mradi wa SGR kwa kuwa Gulwe itakuwa ni stesheni ya Treni ya Mwendokasi na hivyo kutakuwa na watu wengi toka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Nchi kuja Mpwapwa kwa ajili ya shughuli za kiuchumi kupitia treni. Hivyo amewataka wanachi kuwekeze katika kilimo cha mazao ya biashara na chakula, kujenga nyumba bora na za kisasa za kulala wageni, kuwekeza katika hoteli na migahawa iliyoboreshwa, kufanya biashara na shughuli zingine halali.

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri amesema " Wananchi bado hawajalipwa fidia katika maeneo yanayopita reli katika Wilaya ya Mpwapwa ila nawapongeza wananchi wamekuwa waelewa na hawasimamishi shughuli za ujenzi wa reli kwa kuwa hawajapata fidia, kwa hiyo wamekuwa wazalendo". Pia, Mkuu wa Wilaya ameongeza kuwa Wilaya imejipanga kushiriki katika shughuli za kiuchumi kutokana na kuwepo kwa stesheni na reli, kama kuzalisha zao la korosho, alizeti, ufuta na kuanzisha mji wa viwanda katika eneo la Isinghu.

Aidha Mkuu wa Mkoa amemuagiza Mkuregenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndug. Paul Mamba Sweya kupima eneo la Isinghu na kupata vibali ili kuwa eneo la viwanda na viwanja vilivyopimwa ili kuweza kupanga mji na hivyo itapanua ukuaji wa mji wa Mpwapwa. Pia Mkuu wa Mkoa amepongeza maendeleo ya ujenzi wa reli unavyoendea kwa kasi na kwa ustadi mkubwa.


Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usahili MpwapwaDC June 27, 2022
  • Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa May 2022 May 31, 2022
  • Tangazo la kuahirishwa kwa Usahili Halmashauri ya Mpwapwa June 22, 2022
  • Tangazo la Kuahirishwa kwa kikao cha Kamati ya Fedha uongozi na Mipango March 31, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mgao wa Pikipiki Kwa Watendaji wa Kata

    March 01, 2023
  • Mtokeo ya kidato cha nne yatangazwa

    January 29, 2023
  • Matokeo ya Mtihani Darasala nne na Kidato cha Pili 2022

    January 04, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Saba yatangazwa

    December 01, 2022
  • Tazama zote

Video

Video ya Mpango wa Uuzaji wa Viwanja Eneo la Mazae Block "E" katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa -2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
  • Muundo wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani
  • Ratiba ya Vikao vya Madiwani

Viunganishi Linganishi

  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Utumishi portal
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu Teknolojia na Sayansi
  • Sekretarieti ya Ajira

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mpwapwa - Dodoma, Tanzania

    Anwani: S.L.P 12

    Simu: 255 26 2320122/2320

    Simu ya Kiganjani: +255 688639341

    Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovutii

Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.