• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mpwapwa District Council
Mpwapwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
        • Fedha
        • Biashara
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Mali asili
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Usafi na Mazingira
      • Utawala na Utumishi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Habari Mawasiliano na Tehama
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
    • Mamlaka
      • Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mpwapwa
      • Mamlaka ya Maji Mpwapwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashuri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa mbali mbali
    • Fomu za Maombi
    • Miongozo mbali mbali
    • Simulizi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video mbali mbali
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Mkuu Wa Mkoa Atoa Maagizo Mpwapwa

Posted on: July 11th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge ametoa maagizo kadha Wilayani Mpwapwa katika kikao cha Baraza la Hoja lililofanyika leo tarehe 11 Julai 2018 ukumbi wa Mkubwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa. Katika baraza hilo lililohudhuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa Mhe. George Lubeleje, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge,  Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri, Waheshimiwa madiwani, Mkurugenzi Mtendaji, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Wakaguzi wa Nje, na Wakuu wa Idara na Vitengo.

 

Baadhi ya  wajumbe  wakifuatilia kwa umakini baraza la hoja Wilayani Mpwapwa (Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)

Aidha kwa ukagunzi uliofanyika mwaka 2016/2017 Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imepata Hati Safi ambapo Mkuu wa mkoa amepongeza sana kwa kupata hati hiyo ila ametoa tahadhari kwa uongozi wa wilaya ya Mpwapwa kutobweteka kwa hati hiyo na wanapaswa kufanyakazi kwa kufuata taratibu, sheria na kanuni ili kutozalisha hoja zingine.Ameongeza kuwa taratibu zikifuata halmashauri itakuwa haina hoja.

Aidha Mkuu wa Mkoa huyo amesifu kwa namna hoja zilifyojibiwa kwa kubanga hoja, mapendekezo ya mkaguzi, majibu ya menejimenti, mapendekezo ya kamati ya fedha, uongozi na mipango pamoja na mapendekezo ya baraza la hoja.

 Pia Mkuu wa Mkoa ametoa ushauri kwa uongozi wa wilaya ya Mpwapwa kuwa ipange ratiba ya kusikiliza Migogoro yote ya ardhi, kupatiwa ufumbuzi, na kutunza kumbukumbu ya migogoro hiyo,  20% ya vijiji ipelekwe vijijini ikafanye maendeleo ngazi ya vijiji, 10% ya wanawake na vijana pia ipelekwe kwa walengwa na wahamasishwe kuunda vikundi vyenye tija ili waweze kutumia  fedha hizo katika kuleta maendeleo na sio kutumia kwa matumizi binafsi.

Baadhi ya  wajumbe  wakifuatilia kwa umakini baraza la hoja Wilayani Mpwapwa (Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)

Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa Ametoa maagizo yafuatayo kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa:-

 1. Kukusanya mapato kwa kutumia Mashine za Kielektroniki (POS) na kuwachulia hatua kali watu wote wanaohujumu mapato kupitia POS.

 2. Kutohamisha fedha za mradi mmoja na kwenda kwenye mradi mwingine.

 3.Kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuvisimamia kimamilifu ili kuongeza Mapato ya kutosha.

 4. Kuboresha miundombinu ya shule kama vile madarasa.

 5. Viongozi wa Vijiji na mitaa waitishe vikao vya kisheria na wasome mapato na matumizi.

 6. Kuanza kufanya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Disemba 2019.

 7. Viongozi waamasishe wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuupokea mwenge wa uhuru unaotarajiwa kupokelewa kimkoa wilayani Mpwapwa

      tarehe 30 Julai 2018 na kuzindua miradi 6.

8. Kufanya usafi wa mazingira katika maeneo ya makazi na biashara.

9. Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kuhakikisha Wilaya ya Mpwapwa inakuwa salama hasa ukizingatia sasa Dodoma ni Jiji na tunapata wageni wengi

     toka maeneo mbalimbali na nchi jirani.

Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usahili MpwapwaDC June 27, 2022
  • Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa May 2022 May 31, 2022
  • Tangazo la kuahirishwa kwa Usahili Halmashauri ya Mpwapwa June 22, 2022
  • Tangazo la Kuahirishwa kwa kikao cha Kamati ya Fedha uongozi na Mipango March 31, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mgao wa Pikipiki Kwa Watendaji wa Kata

    March 01, 2023
  • Mtokeo ya kidato cha nne yatangazwa

    January 29, 2023
  • Matokeo ya Mtihani Darasala nne na Kidato cha Pili 2022

    January 04, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Saba yatangazwa

    December 01, 2022
  • Tazama zote

Video

Video ya Mpango wa Uuzaji wa Viwanja Eneo la Mazae Block "E" katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa -2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
  • Muundo wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani
  • Ratiba ya Vikao vya Madiwani

Viunganishi Linganishi

  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Utumishi portal
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu Teknolojia na Sayansi
  • Sekretarieti ya Ajira

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mpwapwa - Dodoma, Tanzania

    Anwani: S.L.P 12

    Simu: 255 26 2320122/2320

    Simu ya Kiganjani: +255 688639341

    Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovutii

Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.