(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma Mhe. Godwin Mkanwa ambaye ni kiongozi wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma leo amefanya ziara ya kukagua mradi Skimu ya umwagiliaji Msagali katika Wilaya ya Mpwapwa. Katika ziara hiyo Kamati ya siasa ya Mkoa wa Dodoma imeambatana na Kamati ya siasa ya Wilaya ya Mpwapwa chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Chibwiye, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Donalth S. Nghwenzi na wataalam toka Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa. na Mkoani Dodoma.
Baada ya kuwasili katika skimu ya umwagilia Msagali, Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya MpwapwaNdug. Maria Leshalu alieleza kwa ufupi juu ya skimu. Skimu hii ya umwagiliaji Msagali ipo katika kijiji cha Msagali, kata ya Chunyu, tarafa ya Mpwapwa wilayani Mpwapwa inafaa kwa kilimo cha umwagiliaji kutegemea maji ya mvua yanayotiririka kupitia mto wa msimu wujulikanao kama Kinyasungwi. Skimu inajishughulisha na uzalishaji wa zao la Mpunga ambapo wakulima 297 ndio wenye mashamba yenye ukubwa wa ekari 525 ambalo linamwagiliwa. Kwa ujumla skimu ina ekari 1500 linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji.
Asili ya Mradi huu ni Mwaka 2002 ambapo wafadhili wa Irish Aid, International Fund for Agriculture Development (IFAD), World Food Programme (WFP) pamoja na Serikali ya Tanzaniakwa kupitia program ya PIDP walifanya upembuzi wa kina katika mikoa sita ya Dodoma, Shinyanga, Singida, Arusha, Tabora na Mwanza ambazo zilipelekea kwa Wilaya 12 ambazo zilikidhi vigezo.
Ujenzi wa mradi huu ulikuwa ni wa awamu tano kwa miaka tofauti tofauti:- ujenzi wa banio pamoja na mfereji mkuu (mwaka 2004-2005), Ujenzi na ukarabati wa mfereji mkuu (2007-2008), ujenzi wa mfereji mkuu (2008-2009), ujenzi wa mfereji mkuu pamoja kufanya tafiti za bwawa (mwaka 2010-2011) na Ujenzi wa mifereji ya kati na midogo (mwaka 2013-2014). Ambapokwa ujenzi wote tangu kuanza mwaka 2004 hadi 2014, takribani Tsh. 1,695,816,172 zimeshatumika. Pia imeelezwa kuwa ili mradi huu uwe na tija na kuweza kuazalisha kwa wingi unahitaji takribani shilingi Bilioni kumi na moja.
Mafanikio ya mradi tangu kuanzishwa ni:- kuongezeka kwa uzalishaji kutoka gunia 3 kwa ekari hadi kufikia gunia 10 hadi 15 kwa ekari, kuongezeka kwa wakulima katika skimu yaumwagiliaji kutoka wakulima 30 hadi kufikia wakulima 297 na kuwa na uhakika wa chakula ngazi ya kaya.
Aidha Mkuu wa Msafara wa Kamati ya Siasa ya Mkoa Mhe. Godwin Mkanwa baada ya kupatiwa maelezo mafupi juu ya mradi huu, kwanza amepongeza hatua iliyofikiwa pamoja namafanikio yake. Pia ameongeza kuwa Mkoa wa Dodoma unategemea chakula kutoka Mpwapwa, hivyo kwa mradi huu utazalisha mazao ya chakula kwwingi kama vile mpunga, matunda kama matikiti maji, maboga, mboga za majani. Shughuli zingine ni kama vile ufugaji wa samaki, kupata maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, kunyweshea mifugo na kuthibiti uharibifu wa barabara ya Dodoma - Mpwapwa kwa kuwa maji ya mto yanayootiririka yatahifadhiwa.
Pia Mhe. Mkanwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa ashirikiane na wataalam kuandika andiko ili mradi huu uweze kukamilika na kuleta ufanisi. Pia ameahidi kuwa atawasiliana na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Makame Mbarawa kuja kutembelea skimu hii ili nae aweze kutoa mchango wake katika kusaidia fursa hii.
Akishukuru ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri amesema "Nakushukuru sana Mhe. Mkanwa kwa kuahidi kutuletea Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Makame Mbarawa kuja kuona na kutusaidia, ila Mimi na Mchumi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa tumeshaenda kuwaona wadau mbalimbali juu ya skimu hii wakiwemo Benki ya Dunia na wadau wa mzaingira ili kuthibiti maji ya mto huu ambao unaathiri sana mazingira na barabara ya Dodoma - Mpwapwa, reli na madaraja, hivyo litajengwa bwawa. Pia kati ya mwezi Februari na Machi mwaka huu 2019 mkoa wa Dodoma umeandaa Investment Forum ambapo sisi kama Mpwapwa tumeandaa Miradi ya Uwekezaji ambapo tumeweka Skimu hii ya Msagali na Bonde la Lumuma na tutaenda kulisemea vizuri katika forum hiyo "
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.