Halmahauri ya Wilaya ya Mpwapwa leo imeadhimisha Siku ya Wanawake Dunia kama inavyoadhishwa kila mwaka tarehe 8 Machi. Kwa mwaka huu Siku ya Wanawake imeadhimishwa kwa kupanda miti katika eneo la wazi katika kijiji cha Ilolo kata ya Mpwapwa Mjini. Katika siku hiyo wanawake takribani 150 walijitokeza kuungana na wenzao kutoka majumbani na watumishi kutoka katika taasisi mbalimbali za umma na binafsi. Pia wanaume waliungana na wanawake na kufanya maandamano ya amani hadi katika eneo la kupanda miti.
Kazi ya kupanda miti ilifanywa kwa bidii na juhudi kubwa na kwa muda mfupi kama dakika 45 tu zoezi la upandaji miti lilikamilika na idadi ya miti iliypandwa ilikuwa miche 300 kwa mujibu wa takwimu za Afisa Mazingira Ndugu. Theodory Mulokozi.
Baada ya zoezi hili kukamilika Mkuregenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa alikuwa mgeni rasmi alitoa hotuba fupi juu ya umuhimu wa siku hiyo na jitihada za serikali katika kumkuwamua mwanamke katika uchumi kwa kuweka mazingira wezeshi kama kuanzisha vikundi na kuvikopesha na kuwapa fursa ya kupanga na kujadili mambo yao wenyewe.
Pia mgeni rasmi aliwashukuru wote walihudhuria katika zoezi la upandaji miti na mwisho alimkabidhi mwenyekiti wa kijiji cha Ilolo kuilinda miti hiyo isiweze kuharibiwa na watoto au mifugo.
Mwakilishi wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mpwapwa Akisoma taarifa ya Wanawake Mbele ya Mgeni Rasmi mara tu baada ya kumaliza zoezi la upandaji miti.
Wanawake wa Mpwapwa wakiwa katika maandamano ya amani katika siku ya wanawake duniani kuelekea eneo la upandaji miji katika kijiji cha Ilolo
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.