• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mpwapwa District Council
Mpwapwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
        • Fedha
        • Biashara
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Mali asili
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Usafi na Mazingira
      • Utawala na Utumishi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Habari Mawasiliano na Tehama
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
    • Mamlaka
      • Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mpwapwa
      • Mamlaka ya Maji Mpwapwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashuri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa mbali mbali
    • Fomu za Maombi
    • Miongozo mbali mbali
    • Simulizi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video mbali mbali
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Wazee Wapatiwa Vitambulisho vya Matibabu Bure katika Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani

Posted on: May 15th, 2018

Siku ya Familia Duniani huadhimishwa kila mwaka Mei 15, na Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa. Maadhimisho hayo yanatokana na Tamko la Baraza la Umoja wa Mataifa Na. 47/257 la tarehe 20 Septemba 1993 lililoidhinisha siku maalum kwa ajili ya familia.

Tanzania ni moja  ya Nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa, hivyo huungana na nchi zingine kila mwaka kuadhimisha siku hii. Mwaka huu maadhimisho yanafanyika kiwilaya kwa kuzingatia utaratibu watakao jiwekea na ma mazingira ya Wilaya husika. 

Kwa willaya ya Mpwapwa maadhimisho hayo yamefanyika kwa kuanza na kufanya usafi katika Hospitali ya Wilaya ambapo wananchi na wadau mbalimbali wamehudhuria katika kufanya usafi. Pia maadhimisho hayo yameenda sambamba na Uzinduzi wa Vitambulisho vya Matibabu Bure kwa Wazee.

Mgeni rasmi katika Maadhibisho hayo ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. George Fuime, ametoa hotuba fupi yenye maudhui ya kuhamasisha, kuhimiza, kuelimisha na kuitanabaisha jamii kuhusu umuhimu wa familia na malezi bora kwa watoto ili kupata kizazi cha watoto wenye maadili mema katika jamii.

Mhe. George Fuime (Makamu Mwenyekiti wa Halmashuri ya  Wilaya ya Mpwapwa) akihutubia wananchi katika maadhimisho ya siku ya familia

Aidha Mgeni rasmi amefafanua Kauli mbiu katika ya mwaka 2018 kuwa ni "Malezi Jumuishi ni Msingi wa Uzalendo, Utu na Maadili ya Familia na Taifa" ambayo inalenga kuhamasisha familia umuhimu wa malezi kwa watoto na kutenga muda wa kukaanao kwa pamoja ili kujiepusha na matukio ya ukatili dhidi ya watoto na kuelimisha jamii kuachana na mila  na desturi zenye kuleta madhara pamoja na imani za kishirikiana.

Pia amewakumbusha wanafamilia kutimiza wajibu wao katika upatikanaji wa Elimu na Malezi bora kwa watoto .

Vilevile Mgeni rasmi amezindua viambulisho vya matibabu bure kwa wazee ambapo wazee 170 wa kata ya Mpwapwa mjini wamepatiwa vitambulisho vyao. Aidha amesema zoezi hili la vitambulisho ni endelevu na kwa kuanza tumeanza na kata ya Mpwapwa Mjini na litaendelea katika kata zote za Wilaya ya Mpwapwa.

Mgeni rasmi (wa pili toka kulia ) akikabidhi kitambulisho cha matibabu bure kwa mzee.

Mzee akitoa neno la shukrani kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Uongozi wa Wilaya ya Mpwapwa kwa kuwaona wazee ni azina muhimu na kuwawezesha kupata matibabu bure.

Wazee wakisubiri kupatiwa vitambulisho vyao vya matibabu bure

Baadhi ya vitambulisho vilivyotolewa kwa wazee

Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usahili MpwapwaDC June 27, 2022
  • Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa May 2022 May 31, 2022
  • Tangazo la kuahirishwa kwa Usahili Halmashauri ya Mpwapwa June 22, 2022
  • Tangazo la Kuahirishwa kwa kikao cha Kamati ya Fedha uongozi na Mipango March 31, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mgao wa Pikipiki Kwa Watendaji wa Kata

    March 01, 2023
  • Mtokeo ya kidato cha nne yatangazwa

    January 29, 2023
  • Matokeo ya Mtihani Darasala nne na Kidato cha Pili 2022

    January 04, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Saba yatangazwa

    December 01, 2022
  • Tazama zote

Video

Video ya Mpango wa Uuzaji wa Viwanja Eneo la Mazae Block "E" katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa -2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
  • Muundo wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani
  • Ratiba ya Vikao vya Madiwani

Viunganishi Linganishi

  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Utumishi portal
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu Teknolojia na Sayansi
  • Sekretarieti ya Ajira

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mpwapwa - Dodoma, Tanzania

    Anwani: S.L.P 12

    Simu: 255 26 2320122/2320

    Simu ya Kiganjani: +255 688639341

    Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovutii

Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.