Na: Shaibu J. Masasi; Afisa TEHAMA - Mpwapwa Dc.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndugu. Paul Mamba Sweya amefungua mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari ya Kudumu la Wapiga Kura kwa Awamu ya Pili mwaka huu 2020. Mafunzo haya yamehudhuriwa na Watendaji wa Kata (ARO Kata) 33, Watumiaji wa Mashine za Kuandikisha Wapiga Kura ( BVR Kit Operators) 33 na Waandikishi Wasaidizi 33. Pia mafunzo haya yamehudhuriwa na wawakilishi wawili toka Tume ya Uchaguzi ya Taifa ambao ni wataalamu wa TEHAMA.
Mafunzo hayo yametolewa huku kukiwa na ugonjwa hatari wa COVID 19 unaosababishwa na Virusi vya Corona. Hata hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi Taifa wamewezesha uwepo wa Maji tiririka, sabuni, tishu na barako ili washiriki waweze kujikinga na ugonjwa huo kama wataalam wa afya wanavyoshauri.
Zoezi la Uandikishaji linatarajiwa kuanza tarehe 2 hadi 4, Mei 2020 katika kata zote za Wilaya ya Mpwapwa, hivyo wananchi wahamasishwe kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha na kurekebisha taarifa zao.
Katika hotuba ya Ufunguzi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa amesema "Pamoja na kazi hii nyeti na muhimu, tukiwa katika vituo vya kuandikisha ni bora kila mmoja wetu akajikinga na janga hili la corona kwa kuwa kutakuwa na barakoa kwa ajili ya waandishi na BVR Kit operators, maji tiririka na sabuni. Hivyo kila mtu akija kupata huduma lazima anawe mikono na sabuni. Pia kutakuwa na wahudumu wa afya kwa kila kituo na watawaongoza watu wote kufuata kanuni za afya ili kuepuka kupata maambukizi ya corona na hivyo tunategemea kumaliza kazi salama.
Mwisho Ndugu Sweya amewataka wote walioapishwa kufanyakazi kwa kufuata miongozo na kuwa na nidhamu ya hali ya juu kwa muda wote wa kazi. Pia ameongeza wahusika kutumia lugha nzuri na kutoa elimu kwa wananchi watakaokuja kupata huduma.
Kwa mafunzo ya BVR yametolewa na wataalam wa TEHAMA wa Halmashauri wakishirikiana na Wale wa Tume ya Uchaguzi, hivyo mafunzo yalifanikiwa kwa asilimia 100 kwa kuwa kila mtumiaji wa BVR Kit alifanikiwa, kumsajiri mpiga kura mpya, kurekebisha taarifa za mpiga kura, kutoa kitambulisho na kumfuta mpiga kura katika mfumo.
Hivyo ni matarijio yetu kuwa kazi itafanywa kwa ustadi mkubwa bila makosa yanayoambatana na kutoelewa namna ya kutumia BVR.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.