• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mpwapwa District Council
Mpwapwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
        • Fedha
        • Biashara
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Mali asili
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Usafi na Mazingira
      • Utawala na Utumishi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Habari Mawasiliano na Tehama
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
    • Mamlaka
      • Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mpwapwa
      • Mamlaka ya Maji Mpwapwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashuri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa mbali mbali
    • Fomu za Maombi
    • Miongozo mbali mbali
    • Simulizi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video mbali mbali
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Habari Mawasiliano na Tehama

Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni mojawapo kati ya vitengo vilivyo chini ya  Idara ya Utawala katika  Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

Kitengo hiki kinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Dira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ya kuwa Taasisi inayomjali mteja katika utoaji wa huduma kwa ajili ya maendeleo endelevu ifikapo 2025. Pia inatekeleza Mwelekeo wa halmashauri ya Mpwapwa wa kuwapatia wananchi wake huduma bora za kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia misingi ya utawala bora. Hivyo basi Lengo kuu la kitengo hiki ni kuhakikisha miundombinu ya TEHAMA  katika Halmashauri inakuwa bora na salama katika utoaji wa huduma.

Majukumu ya Kitengo cha TEHAMA

Majukumu ya kitengo cha TEHAMA ni kama ifuatavyo;

  • Kuweka usalama wa hifadhi data.
  • Kutoa huduma za hifadhi data kwa watumiaji.
  • Kusimamia maboresho ya programu za kompyuta kwa wakati.
  • Kusakinisha, kusanidi na kuboresha progrmu za kuzuia virusi vya kompyuta (Install, configure and update antivirus software).
  • Kuelimisha watumiaji masuala mbalimbali yanayohusu usalama, hatari na udhaifu katika mifumo ya TEHAMA.
  • Kukagua mifumo ya TEHAMA mara kwa mara.
  • Kuweka viwango vya usalama na udhibiti katika mifumo ya TEHAMA kwa watumiaji.
  • Kusanifu, kusakinisha na kusanidi miundombinu ya ndani na nje ya mtandao wa kompyuta (Desing, install and configure LAN and WAN infrastructure).
  • Kufanya majaribio ya vifaa vya mtandao wa kompyuta.
  • Kushauri kitaalam katika manunuzi ya vifaa bora na vya kudumu vinavyohusu TEHAMA.
  • Kutengeneza vifaa vyote vya TEHAMA vinapoharibiaka au kutofanyakazi iliyokusudiwa.
  • Kusimamia mifumo ya kompyuta hasa mifumo ya Mapato na Mashinne za Kukusanyia Mapato (Point Of Sales - POS).

 Malengo ya Kitengo kwa Mwaka wa fedha 2015/2016 na 2016/2017

Malengo kwa mwaka wa fedha 2015/2016

Kwa mwaka wa fedha 2015/2016 Kitengo kilijiwekea malengo yafuatayo;

  • Kuboresha  miundombinu ya TEHAMA ifikapo Juni 30,2016.
  • Kuimarisha ufanisi wa ufanyajikazi wa kompyuta kwa Kufanya matengenezo ya mara kwa mara ifikapo Juni 30, 2016.
  • Kuwaelekeza watumiaji namna sahihi ya kutumia kompyuta ili ziweze kudumu kwa muda mrefu ifikapo Juni 30, 2016.
  • Kuongeza mashine za kielektroniki za kukusanyia mapato na kufikia 28 ifikapo June 30, 2016.

Malengo kwa mwaka wa fedha 2016/2017

  •      Kuboresha mawasiliano katika idara zote 13 na videngo 6 ifikapo Juni 30, 2017.
  • Kuboresha  utoaji  wa  huduma katika idara na vitengo kwa kutumia mifumo ya kompyuta ifikapo Juni 30, 2017.
  • Kuboresha  na kuongeza ufanisi wa miundombinu ya TEHAMA ifikapo Juni 30,2017.
  • Kuboresha  mifumo  ya  ukusanyaji  wa  mapato  kwa  kutumia mashine za kielektroniki (POS) kwa kila  kata ifikapo Juni 30, 2017.
  • Kuboresha  upatikanaji  wa  taarifa  sahihi  na  haraka zenye ufanisi kwa kutumia tovuti  na barua pepe za serikali ifikapo Juni 30, 2017.

 Watumishi na Vitendea kazi.

Watumishi

Jedwali hapo chini linaonesha mahitaji na  hali halisi  ya watumishi katika Kitengo cha TEHAMA kwa sasa.

Na

Kada

Mahitaji

Waliopo

Mapungufu

1
Mchambuzi wa mifumo ya Kompyuta (System Analyst II)

2

2

0

2
Fundi sanifu wa Kompyuta (Computer Technician)

1

0

1


Jumla

3

2

1


Pamoja na upungufu wa Mtumishi huyo uliopo, kitengo kimeweza  kutekeleza majukumu yake. Pia kama kungekuwa na vitendea kazi vya kutosha kitengo cha TEHAMA kingeweza kutekeleza majukumu yote ipasavyo (matengenezo ya vifaa vya TEHAMA, kusimami na kufunga LAN).

Vitendea Kazi

Pamoja na upungufu wa vitendea kazi, kitengo kinavyo vitendea kazi kama ilivyoorodheshwa katika jedwali hapo chini;

 Vifaa vya ofisi

Na

Kifaa

Idadi

Hali

Maelezo

1.

Crimping tool

2

Nzima

Inatumika

2.
Computer (Desktop)

1

Nzima

Inatumika

3.
Blower

1

Nzima

Inatumika

4.
Cable strippers

2

Nzima

Inatumika

 

Vifaa vilivyopo havitoshi na hivyo vinaathiri sana utekelezaji wa majukumu, kitengo kimeweka katika mpango wa bajeti ya 2017/2018 kunnua vifaa vya ofisi na vitendea kazi.

 UTEKELEZAJI NA USIMAMIZI WA MIRADI

Kitengo kinaendelea na jukumu lake la kusimamia na kutekeleza miradi ya Miundombinu ya Ndani ya Kompyuta (LAN).

Mradi wa Ufungaji wa Miundombinu ya Ndani ya Kompyuta (LAN )  katika Jengo la

  Kituo Kimoja cha Biashara 

Mradi huu umetekelezwa na umekamilika kwa gharama ya Tsh: 7,732,000/= (Milioni saba laki saba na elfu thelathini na mbili tu) ambazo zilifadhiliwa na Local Investment Climent Project (LIC). Mradi huu ulianza Mwezi Desemba, 2016 na kukamilika mwezi Januari, 2017.

 Mafanikio, Changamoto na Mikakati

 Mafanikio

Kuwezesha kutoa taarifa sahihi na za haraka za kifedha za ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mifumo ya mapato (LGRCIS) na matumizi (EPICOR 09).

Kutoa risiti na nyaraka mbalimbali za kifedha zinapohitajika.

Kufuatilia na kuangalia mapato yaliyokusanywa kwa kutumia POS zilizogawanywa kwa watendaji.

Kuthibiti au kupunguza makosa yaliyojitokeza katika ukusanyaji wa kawaida kwa kutumia vitabu .

Kuwawezesha walipa bili kulipa na kuangalia bili zao za huduma mbalimbali kama vile leseni za biashara, kwa kutumia simu za kiganjani iliyounganishwa na NMB mobile kwa kuwa LGRCIS (Local Government Revenue Collection Information System) imeunganishwa na CCS (Cash Collection System).

Kutunza kumbukumbu za mapato na taarifa za walipa bili.

Kupungua kwa vifaa vya TEHAMA visivyofanyakazi kwa kuwa matengenezo huwanywa mara kwa mara.

Kuongezeka kwa ustadi wa watumiaji wa kompyuta na mifumo ya kompyuta baada ya kutoa maelekezo sahihi ya utumiaji wa kompyuta kwa watumiaji hao.

Kupungua kwa changamoto za upotevu wa taarifa miongoni wa watumiji wa kompyuta.

 Changamoto 

  • Ufinyu wa bajeti, kitengo cha TEHAMA kinategemea sana mapato ya ndani na hivyo
  •        kuathiri utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kitengo kwa kuwa fedha hizo
  •       hazitoshelezi.
  • Ukosefu wa fedha ya kuhudhuria mafunzo ya TEHAMA kikamilifu endapo kama mafunzo yanahitaji Halmashuri kugharimia, hii ni kutokana na ukosefu wa fedha.
  • Halmashauri haina Computer Server ambayo ingeweza kuhidhari baadhi ya taarifa muhimu.
  • Ukosefu wa Internet  husababisha taarifa mbalimbali zinazotumwa nje ya Halmashauri kuchelewa.

Mikakati ya kupambana na Changamoto

  • Kuongeza jitihada za kubuni njia mbalimbali za kukusanya mapato ili kuwa na fedha za kutatua changamoto.
  • Kuomba nyaraka kwa maafisa TEHAMA wenzetu waliohudhuria mafunzo mbalimbali na kusoma ili kutatua changamoto za mifumo.
  • Kuomba msaada wa kitaalam katika kitengo cha TEHAMA kilichopo ofisi ya TAMISEMI.
  • Kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya kulipa ushuru na matumizi sahihi ya mashine za kielektroniki za kukusanyia mapato (POS).
  • Kuendelea kuongeza mashine za kielektroniki za kukusanyia mapato (POS).
  • Kuendelea kushirikiana na idara na vitengo vinavyotumia kompyuta ili kupata taarifa kama kutakuwa na matatizo ya kiufundi ili yaweze kutatuliwa mara moja.
  •  Ili kupunguza tatizo la internet , mchakato wa kufunga wired na wireless router kupitia kampuni ya TTCL (Tanzania Telecomunication Limited) unaendelea, ambayo itawezesha kutoa huduma ya internet kwa gharama nafuu katika Halmashauri ya Mpwapwa.

Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usahili MpwapwaDC June 27, 2022
  • Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa May 2022 May 31, 2022
  • Tangazo la kuahirishwa kwa Usahili Halmashauri ya Mpwapwa June 22, 2022
  • Tangazo la Kuahirishwa kwa kikao cha Kamati ya Fedha uongozi na Mipango March 31, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mgao wa Pikipiki Kwa Watendaji wa Kata

    March 01, 2023
  • Mtokeo ya kidato cha nne yatangazwa

    January 29, 2023
  • Matokeo ya Mtihani Darasala nne na Kidato cha Pili 2022

    January 04, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Saba yatangazwa

    December 01, 2022
  • Tazama zote

Video

Video ya Mpango wa Uuzaji wa Viwanja Eneo la Mazae Block "E" katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa -2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
  • Muundo wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani
  • Ratiba ya Vikao vya Madiwani

Viunganishi Linganishi

  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Utumishi portal
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu Teknolojia na Sayansi
  • Sekretarieti ya Ajira

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mpwapwa - Dodoma, Tanzania

    Anwani: S.L.P 12

    Simu: 255 26 2320122/2320

    Simu ya Kiganjani: +255 688639341

    Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovutii

Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.