• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mpwapwa District Council
Mpwapwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
        • Fedha
        • Biashara
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Mali asili
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Usafi na Mazingira
      • Utawala na Utumishi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Habari Mawasiliano na Tehama
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
    • Mamlaka
      • Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mpwapwa
      • Mamlaka ya Maji Mpwapwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashuri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa mbali mbali
    • Fomu za Maombi
    • Miongozo mbali mbali
    • Simulizi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video mbali mbali
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Usafi na Mazingira

USAFI WA MAZINGIRA

Halmashauri kupitia Idara ya usafi na Mazingira inaendelea kusimamia utunzaji na udhibiti wa uharibifu wa mazingira ndani ya wilaya. Hadi sasa watuhumiwa 65 wamebainishwa na kuthibitika kufanya uharibifu wa mazingira kati yao watuhumiwa 8 wamelipa faini tayari na watuhumiwa 2 wamefungwa gerezani. Pamoja na hatua hizo bado taratibu za kuwafikisha kwenye mabaraza ya kata watuhumiwa waliobaki zinaendelea na ufuatiliajiunaendelea.

 Uzoaji wa taka ngumu – juhudi kubwa zimefanywa na idara kuhakikisha taka zote zinazozalishwa zinakusanywa na kusafirishwa, kutumia gari la Halmashauri na magari ya wadau mbalimbali wa Halmashauri.

Halmashauri inaendelea kusimamia usalama wa afya mazingira na kudhibiti milipuko ya magojwa itokanayo na uchafu wa mazingira.

MAJUKUMU YA IDARA KWA UJUMLA

  • Idara inajukumu kubwa la kuhakikisha ulinzi na usimamizi wa raisilimali za mazingira vinasimamiwa kwa maendeleo endelevu.
  • Kudhibiti uharibifu wa mazingira kwa namna yoyote na kuchukua hatua madhubuti za kisheria dhidi ya waharifu.
  • Kuhakikisha kanuni za afya zina zingatiwa mahali popote ndani ya wilaya ili kuepuka magonjwa ya milipuko yatokanayo na uchafu
  • Kuhakikisha uulinzi na usalama wa afya ya jamii katika bidhaa na huduma mbalimbali za kijamii.
  • Kusimamia usafi wa mazingira, uzoaji wa taka , na utupaji salama wa taka katika maeneo yaliyo ainishwa kwa shughuli hiyo
  • Idara inajukumu la kusimamia utekelezaji sera, sheria , taratibu na miongozo yote inayohusu afya ya jamii na usimamizi wa mazingira katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.
  • Idara inajukumu kubwa la kutoa elimu, na kuweka mikati madhubuti ya kukabiliana na majanga ya asili na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia ya nchi.

 HALI YA WATUMISHI

Idara ina jumla ya watumishi 11 wa kada mbili, watumishi 9 kutoka kitengo cha Usafi na 2 kitengo cha Mazingira.

Jedwali No. 1 WATUMISHI

NA
KADA
MAHITAJI
WALIOPO
UPUNGUFU
1
MKUU WA IDARA
1
1
0
2
USAFI
36
9
27
3
MAZINGIRA
36
2
34

MUUNDO WA IDARA

Idara ya Usafi na Mazingira imegawanyika katika vitengo viwili yaani kitengo cha USAFI na kitengo cha MAZINGIRA.

  •  KITENGO CHA MAZINGIRA

Kitengo hiki kina wajibika kutekeleza majukumu mbalimbali kama ifuatavyo

  • kuhakikisha utekelezaji wa Sheria ya usimamizi wa mazingira kwenye eneo zima la Halmashauri ya Mpwapwa
  • kushauri Menejiment na Kamati ya Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri kuhusu masuala yote ya mazingira
  • kukuza weledi kuhusu ulinzi wa mazingira na uhifadhi maliasili kwenye Halmashauri
  • kukusanya na kusimamia taarifa kuhusu mazingira na matumizi ya maliasili ndani ya Halmashauri
  • kuandaa taarifa za mihula kuhusu hali ya mazingira ndani ya Wilaya
  • kufuatilia maandalizi, mapitio na vibali vya Tathmini ya Athari kwa Mazingira kwa ajili ya uwekezaji wa ndani wa miradi mbalimbali
  • kufanya mapitio ya sheria ndogo zinazohusu usimamizi wa mazingira na shughuli maalumu za kisekta zinazohusiana na mazingira;
  • kutoa taarifa kwa Mkurugenzi wa Mazingira na Mkurugenzi Mkuu kuhusu utekelezaji wa Sheria ya usimamizi wa mazingira.
  • Kutoa (disseminate) Elimu ya Hifadhi ya Mazingira kwa wadau mbalimbali.
  • Kushiriki katika kuandaa mpango kazi na Bajeti.
  • Kushiriki katika tafiti zinazohusu usimamizi na Hifadhi ya Mazingira.
  • Kufuatilia na kuainisha maeneo yanayopaswa kuhifadhiwa.
  • Kufanya ukaguzi wa usafi katika maeneo ya mji, mtaa, kaya kama sheria, kanuni na miongozo inavyoelekeza.
  • Kuhimiza na kuratibu zoezi la ukusanyaji wa taka ngumu na kuzitupa kwenye maeneo tengwa eg.dampo.
  • Kusimamia uundwaji wa kamati za mazingira na kuziimarisha katika ngazi zote za kiutawala

B: KITENGO CHA USAFI NA AFYA YA JAMII

Kitengo cha usafi na afya ya jamii kina majukumu yafuatayo

  • kuratibu zoezi la ukusanyaji wa taka ngumu na kuzitupa kwenye maeneo tengwa eg.dampo.
  • Kuratibu zoezi la utupaji wa taka maji katika halmashauri ya Mpwapwa
  • Kutoa elimu ya afya kwa jamii juu ya usafi na magonjwa ya kuambukizwa yatokanayo na usafi
  • Kusimamia utekeleza wa sheria, sera, taratibu na miongozo mbalimbali ya afya jamii katika halmashauri ya Mpwapwa
  • Kuratibu na kufanya kazi mbalimbali kwenye maeneo yaote yanayohusu huduma za kijamii ( taasisi, maduka, holeli, migahawa, viwanda , nyumba za kuishi na nyuma za wageni)
  • Kukagua ramani za majengo mbalimbali kuhakisha uwepo wa mifumo sahihi ya utupaji taka ngumu na taka maji.
  • kuandaa taarifa za mihula zinazohusu masuala ya afya ya jamii ndani ya Wilaya
  • kusikiliza kero mbalimbali za wananchi zinazohusu afya ya jamii ndani ya wilaya ya Mpwapwa.
  • kuandaa mipango na mikakati kudhibiti na kupambana na magonjwa ya milipuko ndani ya wilaya
  • kuratibu uundawaji,na usimamizi wa klabu za mtoto kwa mtoto za usafi wa mazingira mashuleni
  • kuratibu, na kusimamia kampeni ya usafi na mazingira ya kitaifa ndani ya wilaya ya Mpwapwa( ujenzi wa vyoo bora, uwekaji wa vibuyuchirizi, vichanja na uchimbaji mashimo ya taka)
  • kuratibu na kusimamia mradi wa Saro tap (hand washing facility kwenye mashule na taasisi binafsi na serikali.

 MIKAKATI YA IDARA 

Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kupitia Idara ya Usafi na Mazingira imejiwekea mikakati mbalimbali ili kuboresha utunzaji wa mazingira na afya ya jamii. Mikakati hiyo ni pamoja na;- 

1. Kuhakikisha kwamba elimu juu ya Hifadhi ya mazingira na afya ya jamii kwa wadau mbalimbali inafanyika mara kwa mara ilikupunguza au kuondoa kabisa tatizo la uharibifu wa mazingira magonjwa ya milipuko katika Wilaya.

2. kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa mazingira no 20 ya 2004 na marekebisho yake ya 2016 dhidi ya waharibifu wa mazingira, na ukiukwaji wa sheria ya afya ya jamii na 1 ya 2009 dhidi ya wale wote wanaoenda kinyume na kanuni, taratibu na miongozo ya afya ya jamii.

3. Kufuatilia na kuainisha maeneo yanayopaswa kuhifadhiwa kama maeneo yenye chepechepe za maji (Aridhi oevu), kandokando mwa kingo za mito, milima ya hifadhi ya jamii, na maeneo mengine yenye thamani mbalimbali ya uhifadhi.

4. Kuboresha taaluma ya watumishi pamoja na maslahi.

5. kuandaa mikakati na mipango mbalimbali ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira kama programu za upandaji miti.

6. kufuatilia maandalizi, mapitio na vibali vya Tathmini za athari za mazingira zina fanyika kwa miradi mikubwa ya uwekezaji kama vile miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji, Mashule, Minara, uchimbaji wa madini na pia wachimbaji wadogo wa madini kuhakikisha wa mipango ya ulinzi wa mazingira (EPP) na mipango ya usimamizi wa mazingira yaani (EMP) kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa Mazingira na 20 ya 2004 na sheria ya madini na 14 ya 2010.

7. Kuunda kamati za kuhifadhi mazingira kuanzia ngazi ya vijiji,kata na wilaya pamoja na klabu za mtoto kwa mtoto mashuleni.

8. Kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi kwa viongozi, watendaji na kamati za Mazingira.

9. Kutoa Elimu ya afya katika jamii, juu ya kanuni za afya, ujenzi wa vyoo na unawaji mikono, ukusanyaji wa taka Ngumu na za hatari katika maeneo yao, athari za bidhaa zilizokwisha muda wake na usafi wa maeneo ya kutolea huduma kama vile bucha, maduka nyumba za wageni nyumba za kuishi, zahanati , shule, vyuo mashine za nafaka,na migahawa.

10. kuandaa maandiko mbalimbali yanayohusu uhifadhi wa mazingira na afya ya jamii ndani ya Wilaya ya Mpwapwa.

BAADHI YA SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA WANCHI WA MPWAPWA KUHARIBU MAZINGIRA NA VYANZO VYA MAJI

Pic: Uharibifu wa mazingira kwa shughuli za kilimo na mifugo safu za milima wotta kijiji cha Mzase kata ya berege

Pic:Usimamizi na utoaji elimu kuhusu utunzaji wa vyanzo vya maji kitogoji cha kwamdyanga Mpwapwa mjini safu za milima Kiboriani (kwamdyanga water intake)

Pic: kiwanda kidogo cha uchenjuaji wa kopa katika machimbo ya madini ya kopa Tambi kata ya Matomondo (ushauri kuhusu uandaaji wa mipango ya ulinzi wa mazingira – EPP na EMP)

Pic: madini ya kopa yaliyochimbwa tayari kwa usafirishaji katika machimbo ya Tambi kata matomondo

Pic: Mgodi wa machimbo ya kopa Tambi kata ya matomondo

Pic : machimbo ya Kopa katka mgodi wa Rudi kata ya Rudi

Pic: utoaji wa elimu kuhusu uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji ( WDC 2 za Kingiti na Mwanawotta) zilikutanishwa katika chanzo cha maji ili kujionea uharibifu na kupewa elimu ya uhifadhi na Afisa mazingira pamoja na Mhandisi wa Maji Mpwapwa.

Pic : kamati ya mazingira Kijiji cha Mtamba Kata ya Rudi.baada ya kufanya ukaguzi wa maeneo ya hifadhi za milima na vyanzo vya maji Pamoja na afisa Mazingira Mpwapwa watatu toka kushoto.

Pic : maeneo ya milima na vyanzo vya maji Kijiji cha Mtamba Kata ya Rudi yaliyoharibiwa na kulimwa kilimo cha ufuta.

Pic: Uwezeshaji wa kamati ya mazingira kijiji cha Mtamba Kata ya Rudi chini ya Afisa Mazingira na Afisa afya mazingira watatu toka kulia.

Pic: shuguli za kulinda na kutoa elimu ya afya ya jamii, baada ya maafisa afya mazingira kukamata nyama isiyofaa kwa matumizi ya binadamu kwenye bucha. Pichani ni wanafunzi wa chuo cha mifugo Visele wakishuhudia utupwaji wa nyamba iliyokamatwa mabuchani Mpwapwa.

Pic: Shughuli za utekelezaji wa kampeini ya usafi wa mazingira(national sanitation campaign) kuhimiza ujenzi wa vyoo katika kijiji cha Kimagai kata ya Kimagai. Pichani ni zoezi la uchefushaji washiriki wakichora Ramani ya kijiji na kuonyesha maeneo ya vichaka na misutu watu wasio na vyoo wanakojisaidia

Uwekaji wa vifaa bora vya unawaji mikono katika taasisi na mashule na maeneo ya huduma za jamii za unawaji mikono (SARO TAP DESIGN)

Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usahili MpwapwaDC June 27, 2022
  • Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa May 2022 May 31, 2022
  • Tangazo la kuahirishwa kwa Usahili Halmashauri ya Mpwapwa June 22, 2022
  • Tangazo la Kuahirishwa kwa kikao cha Kamati ya Fedha uongozi na Mipango March 31, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mgao wa Pikipiki Kwa Watendaji wa Kata

    March 01, 2023
  • Mtokeo ya kidato cha nne yatangazwa

    January 29, 2023
  • Matokeo ya Mtihani Darasala nne na Kidato cha Pili 2022

    January 04, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Saba yatangazwa

    December 01, 2022
  • Tazama zote

Video

Video ya Mpango wa Uuzaji wa Viwanja Eneo la Mazae Block "E" katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa -2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
  • Muundo wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani
  • Ratiba ya Vikao vya Madiwani

Viunganishi Linganishi

  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Utumishi portal
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu Teknolojia na Sayansi
  • Sekretarieti ya Ajira

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mpwapwa - Dodoma, Tanzania

    Anwani: S.L.P 12

    Simu: 255 26 2320122/2320

    Simu ya Kiganjani: +255 688639341

    Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovutii

Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.